Kiunzi nje
Kiunzi nje ni ganda au ngozi imara inayobeba na kulinda mwili wa mnyama kwa nje, si kwa ndani kama kiunzi cha mifupa.
Wadudu na arthropodi
haririNi hasa wanyama wa ngeli ya arthropodi kama vile wadudu, buibui na kaa wenye kiunzi nje imara ya chitini.
Tofauti ni matumbawe ambao wanakaa pamoja kwa vikundi vikubwa ilhali kila mmoja anajijengea kihunzi nje kidogo na viunzi hivyo vinabaki baada ya tumbawe kufa lakini wengine hujenga juu ya viunzi vya watangulizi: hivi kujenga mwamba tumbawe ambaye yamekuwa chanzo cha visiwa vingi.
Kwa mnyama mdogo kiunzi hicho bado ni laini lakini kinazidi kuwa kigumu. Baada ya muda kama mnyama anaendelea kukua ganda hili gumu linakuwa dogo. Hapo wanyama wenye kiunzi nje hutupa ganda na kukuza ngozi mpya itakayokuwa gumu tena.
Watu na kiunzi nje
haririWatu walianza kuiga mfumo wa wadudu kwa kujitengenezea aina ya kiunzi nje.
Tangu kale wanajeshi waliwahi kuvaa suti za chuma au bapa mbalimbali za metali zilizokinga kifua, kichwa na tumbo.
Katika tiba kama mguu umevunjika unafunikwa bendeji ya plasta itakayokuwa mgumu; kwa muda ni ganda la nje linalobeba uzito wa mwili badala ya mfupa unaoendelea kupona.
Katika teknolojia ya kisasa wahandisi wanachunguza suti za kuvaa kwa wajeruhiwa au walemavu zitakazowawezesha kutembea tena.
Viungo vya Nje
haririBiolojia
hariri- Geometry and Pattern in Nature 3: The holes in radiolarian and diatom tests Ilihifadhiwa 16 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine.
Teknolojia
hariri- Bionic Boots Ilihifadhiwa 18 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- PowerSkip Ilihifadhiwa 5 Oktoba 2010 kwenye Wayback Machine.
- Berkeley Lower Extremity Exoskeleton (BLEEX) Ilihifadhiwa 24 Septemba 2010 kwenye Wayback Machine.
- University of Washington Exo Arm Project Ilihifadhiwa 26 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiunzi nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |