Kizambarau
Kizambarau | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kizambarau wa kawaida (Amblyodipsas polylepis)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 9:
|
Vizambarau ni nyoka wenye sumu wa jenasi Amblyodipsas katika familia Lamprophiidae. Asili ya jina lao ni rangi yao.
Nyoka hawa ni warefu kiasi, zaidi m moja kwa kipeo lakini chini ya sm 60 kwa kawaida. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia yenye mng'ao zambarau, hasa wakiwa wameambua ngozi hivi karibuni. Pengine rangi ya tumbo ni pinki au hudhurungi na spishi kadhaa zina milia njano.
Vizambarau huchimba ndani ya ardhi lakini wanaweza kuwinda juu ya ardhi. Hula nyoka wengine, mijusi na mijusi-nyungunyungu.
Chonge ni meno marefu ya nyuma yenye mifuo. Nyoka hawa wanaweza kung'ata lakini hakuna ripoti za dalili za kusumu katika watu. Hata hivyo wanafanana na nyoka wachimbaji na kwa hiyo jitahadhari.
Spishi
hariri- Amblyodipsas concolor, Kizambarau wa Natal (Kwazulu-Natal purple-glossed snake)
- Aparallactus dimidiata, Kizambarau wa Mpwapwa (Mpwapwa purple-glossed snake)
- Amblyodipsas katangensis, Kizambarau wa Katanga (Katanga purple-glossed snake)
- Amblyodipsas microphthalma, Kizambarau Macho-madogo (Eastern purple-glossed snake)
- Amblyodipsas polylepis, Kizambarau wa Kawaida (Common purple-glossed snake)
- Amblyodipsas rodhaini, Kizambarau wa Rodhain (Rodhain's purple-glossed snake)
- Amblyodipsas teitana, Kizambarau wa Taita (Taita purple-glossed snake)
- Amblyodipsas unicolor, Kizambarau Magharibi (Western purple-glossed snake)
- Amblyodipsas ventrimaculata, Kizambarau wa Kalahari (Kalahari purple-glossed snake)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kizambarau kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |