Köln
Köln (pia: Kolon, kutokana na Kiingereza Cologne; kwa Kijerumani cha kienyeji: Kölle) ni mji wa Ujerumani kando ya mto Rhine wenye wakazi 970,000.
Köln | |||
| |||
Mahali pa mji wa Köln katika Ujerumani |
|||
Majiranukta: 50°56′0″N 6°57′0″E / 50.93333°N 6.95000°E | |||
Nchi | Ujerumani | ||
---|---|---|---|
Jimbo | Rhine Kaskazini - Westfalia | ||
Idadi ya wakazi (2019) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 1.087.863 | ||
Tovuti: www.koeln.de |
Historia
haririMaana asili ya jina ni "koloni". Ni mji wa kale ulioundwa kwa jina la "Colonia Claudia Ara Agrippinensis" kama koloni ya Waroma wa Kale mnamo mwaka 50. Mahali pa mji paliwahi kuwa boma la Kiroma na kabla ya hapo kijiji cha kabila cha Waubii.
Köln ni mji mkubwa wa nne wa Ujerumani na mji mkubwa wa jimbo la Rhine Kaskazini - Westfalia (Nordrhein-Westfalen).
Kuna kanisa kubwa kuliko yote ya Ujerumani ("Kölner Dom") ambalo ni maarufu kwa sababu limejengwa katika muda wa miaka 700 tangu mwaka 1248 hadi 1880. Masalia ya mamajusi watatu waliomtembelea mtoto Yesu huko Bethlehemu yanasemekana kutunzwa humo. Köln ni kitovu muhimu wa Kanisa Katoliki nchini na makao wa askofu mkuu.
Chuo kikuu chake kilianzishwa mwaka 1388 na leo kuna wanafunzi 44,000 na pamoja na vyuo vingine kuna wanafunzi zaidi ya 80,000 kwenye ngazi ya vyuo. Kati ya vyuo vingine Chuo cha Muziki kimejulikana sana kimataifa.
Mji umejulikana pia kwa aina yake ya pekee ya bia.
Köln ni pia kitovu cha Waafrika katika Ujerumani. Pamoja na wanafunzi wengi kutoka Afrika kuna pia taasisi kama huduma ya Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) zinazoajiri Waafrika wengi. Kuna hata vilabu ambako bia aina ya Tusker kutoka Kenya inauzwa.
Mwaka 2005 Köln ilikuwa mahali pa Siku ya kimataifa ya vijana Wakatoliki; zaidi ya milioni moja walikutana na Papa Benedikto XVI.
Watalii wengi wanafika kila mwaka kwa sherehe ya Karnivali kabla ya majira ya Kwaresima.
Picha
haririTazama pia
haririViungo vya Nje
hariri- German page on the city
- German page of the University
- German page of the cathedral
- German page of the broadcasting station Westdeutscher Rundfunk
Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Köln kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |