Kononi mtunzabustani

Kononi mtunzabustani (Nazareth, Israeli, karne ya 3 - Pamfilia, leo nchini Uturuki, 250 hivi) alikuwa mkaapweke ambaye alijipatia chakula kutokana na bustani na hatimaye aliuawa kwa imani ya Kikristo wakati wa dhuluma ya kaisari Decius wa Dola la Roma[1].

Sehemu ya picha takatifu anamoonekana.

Wakati wa kuhojiwa alijitambulisha kama mtu wa ukoo wa Yesu Kristo. Alipigiliwa misumari miguuni akalazimishwa kukimbia mbele ya gari la kukokotwa hadi alipoanguka magotini na kufa akisali.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 5 Machi[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.