Koti (kutoka Kiingereza: coat)) ni vazi linalovaliwa na jinsia yoyote kwa minajili ya kupata joto na pia kwa uanamitindo (fasheni).

Mwanamume akiwa amevalia koti ndefu.
Mwanamke akiwa amevalia koti aina ya zippileather.

Koti huwa na mikono mirefu (long sleeve) na huwa wazi kwa upande wa mbele ambapo waweza kufunga kwa kutumia vifungo, mnyororo au mshipi. Koti pia huenda ikawa na kofia au hoodie ya kuvalia kichwani.

Historia ya koti

hariri

Kamusi ya Kiingereza ya Oxford ina ithibati kwamba vazi hilo lilianza kuvaliwa tangu karne ya 13 ambapo jina coat lilikuwa likiandikwa kama cote. Jina coat linatokana na lugha ya Kifaransa na Kiitalia.

Katika Karne za Kati na renaissance, koti lilikuwa na urefu wa wastani, lenye vifungo kwa upande wa mbele na lenye skati yake iliyokuwa lazima iambatane na koti lenyewe. Hivi leo, hili halipo.

Aina za koti leo

hariri
 
Koti la suti
 
Fur hooded coat
 
Koti la kujikinga na mvua
 
Trench coat

Hivi leo, kuna koti aina nyingi, kama vile:

  1. Kuna koti la suti ambalo huvaliwa na suruali yenye rangi na muundo sawa na koti.
  2. Kuna koti lenye kofia yenye manyoya kwa kichwa ambalo huvaliwa na walio kwenye nchi zenye baridi jingi.
  3. Kuna koti ndefu linaloitwa trench coat ambalo hufungwa kwa mshipi huku mbele
  4. Kuna koti la ngozi (leather) ambalo hutengenezwa kwa ngozi ya wanyama kama ng'ombe, nyoka au mamba na limekuwa la kufana sana, haswa kwa watu wa pikipiki ambao wanahitaji kujikinga dhidi ya baridi na upepo wanapoendesha vyombo vyao.
  5. Kuna koti la nailoni ambalo huvaliwa wakati wa mvua kujikinga kutokana na kurowa maji yaani rain macs
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Koti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.