Kotwe
Kotwe | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kotwe
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nususpishi 2:
|
Kotwe au bata kotwe (Thalassornis leuconotus) ni ndege wa maji na spishi pekee katika nusufamilia Thalassorninae ya familia Anatidae. Anatokea kwa asili katika Afrika tu, lakini amewasilishwa katika mbuga na hifadhi katika nchi nyingine.
Kotwe huonekana wafupi na wanene. Rangi yao ya msingi ni hudhurungi lakini wana madoa meusi kwenye mabawa na mgongo na madoa meusi madogo kwenye sehemu nyingine za mwili. Domo ni jeusi wenye madoadoa njano na miguu ni kijani-kijivu. Upande wa chini wa mgongo ni mweupe na kuna baka jeupe pande zote mbili karibu na domo. Madume na majike wanafanana. Wote hukua hadi urefu wa sm 45 na uzito wa g 625 hadi 800. Wametoholewa vizuri kwa kuzama na wanaweza kukaa chini ya maji kwa takriban nusu dakika na kuenda hadi m 65 hapo. Wakiogelea mkia umelala juu ya maji.
Chakula chao ni sehemu za mimea ya maji, haswa mbegu na majani. Wanapenda sana viazi vya myungiyungi. Makinda hula viwavi na lava za wadudu pia. Tago hujengwa kwa vijiti na mimea ya maji juu ya visiwa vidogo au kati ya mitete. Jike hutaga mayai 4-10 ya hudhurungi.
Nususpishi
hariri- Thalassornis l. insularis, Kotwe wa Madagaska (Madagaska)
- Thalassornis l. leuconotus, Kotwe wa Afrika (Bara la Afrika)