Kylian Hazard (alizaliwa 5 Agosti 1995) ni mchezaji wa soka ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa klabu ya Cercle Brugge. Ana kaka wawili, Eden na Thorgan, na mdogo mmoja, Ethan, wote ni wacheza mpira.

Huyu ni Kylian Hazard

Kazi ya klabu hariri

Újpest hariri

mnamo 27 Juni 2015, Hazard alisaini mkataba wa miaka mitatu na upande wa Hungary katika klabu ya Újpest. Hazard alicheza kwa mara ya kwanza tarehe 18 Julai 2015 dhidi ya Paksi FC ambayo ilimalizika kwa sare ya 0-0.Tarehe 21 Novemba 2015, Hazard alifunga goli lake la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Honvéd.

Chelsea F.C. hariri

Mnamo tarehe 29 Agosti 2017, Kylian alijiunga na Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, na akawekwa katika kikosi cha klabu Chelsea na alikubali mpango mpya wa miaka miwili na alitumwa kwa klabu ya Cercle Brugge kwa mkopo wa muda mrefu.

Cercle Brugge hariri

Mnamo tarehe 5 Mei 2019, ilitangazwa kuwa Kylian Hazard katika klabu ya Cercle Brugge ni mchezaji wa kudumu na si wa mkopo tena.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kylian Hazard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.