07°39′47″S 36°58′39″E / 7.66306°S 36.97750°E / -7.66306; 36.97750 Lambo la Kidatu ni lambo la TANESCO lililojengwa miaka ya 1970 kwenye mto Ruaha Mkuu katika mkoa wa Morogoro (Tanzania) ili maji yake yaweze kutumika kuzalisha umeme.

Ndilo lambo ambalo ni asili ya sehemu kubwa ya umeme wa taifa.

Kituo cha umeme cha Kidatu kilijengwa hadi mwaka 1975 kama sehemu ya mradi unaoitwa "Mradi wa umeme wa Ruaha Kuu" ulioendelea baadaye kwa ujenzi wa Lambo la Mtera kilomita 170 juu ya Kidatu[1].

Lambo la Kidatu lina urefu wa mita 350 na kimo cha mita 40. Lilijengwa kwa kutumia 40,000 za zege pamoja na 800,000 za udongo na mawe. Inaweza kushika hadi m³ milioni 125 za maji kwa kusudi la kuzipitisha kwa njia ya mabomba yenye urefu wa jumla ya kilomita 10 kwenda rafadha zinazosukuma jenereta 4 zenye uwezo wa kuzalisha megawati 200[2].

Tanbihi

hariri
  1. Yawson, Kongo, Kachroo: Impact Assessment of Mtera and Kidatu Reservoirs on the Annual Maximum Floods at Stiegler’s Gorge of the Rufiji River in Tanzania, Water International, Volume 31, Number 1, Pages 100–108, March 2006, iliangaliwa Mei 2018
  2. Kidatu Hydro Power Plant Archived 27 Desemba 2017 at the Wayback Machine., tovuti ya TANESCO, iliangaliwa Mei 2018

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lambo la Kidatu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.