Kidatu ni kata ya Wilaya ya Ifakara Mjini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67508.

Kidatu

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 27,463 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 32,589 [2] walioishi humo.

Iko kando ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa iliyopo upande wa kaskazini karibu na mto Ruaha Mkuu, pale inapotoka milimani na kuingia katika tambarare ya Kilombero. Milima hiyo inasaidia kuongeza uchumi wa taifa kwa sekta ya utalii hapa nchini.

Inapakana na hifadhi ya wanyama ya Selous upande wa kusini.

Uchumi hariri

Uchumi ya wakazi hutegemea kilimo. Ajira inapatikana kwenye mashamba ya sukari ya Illovo.[3]

Kuna pia kiwanda cha sukari cha Illovo.[4]

Lambo la Kidatu la TANESCO ambalo lipo karibu ni asili ya sehemu kubwa ya umeme kwa taifa.

Usafiri hariri

Kidatu ni mahali ambako reli za TAZARA na Reli ya Kati huunganishwa kwa njia ya reli kutoka Kilosa. Kuna mitambo ya kubadilisha magari ya reli kutoka upana mkubwa wa reli ya TAZARA na upana mdogo wa Reli ya Kati.

Pia kuna barabara inayounganisha kata hiyo na wilaya ya Kilosa na kata nyingine za wilaya ya Kilombero[5][6].

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Kata za Wilaya ya Ifakara Mjini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Ifakara | Katindiuka | Kibaoni | Kiberege | Kidatu | Kisawasawa | Lipangalala | Lumemo | Mang'ula | Mang’ula 'B' | Mbasa | Michenga | Mkula | Mlabani | Msolwa Station | Mwaya | Sanje | Signal | Viwanjasitini


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kidatu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.