Lanthanidi

Namba atomia Elementi ya kikemia Alama Picha
57 Lanthani La Lanthanum-2.jpg
58 Ceri Ce Cerium2.jpg
59 Praseodimi Pr Praseodymium.jpg
60 Neodimi Nd Neodymium2.jpg
61 Promethi Pm
62 Samari Sm Samarium-2.jpg
63 Europi Eu Europium.jpg
64 Gadolini M-ngu Gadolinium-3.jpg
65 Terbi Tb Terbium-2.jpg
66 Disprosi Dy Dy chips.jpg
67 Holmi Ho Holmium2.jpg
68 Erbi Er Erbium-crop.jpg
69 Thuli Tm Thulium sublimed dendritic and 1cm3 cube.jpg
70 Ytebi Yb Ytterbium-3.jpg
71 Luteti Lu Lutetium sublimed dendritic and 1cm3 cube.jpg

Lanthanidi (lanthanide, pia lanthanoidi) ni kundi la elementi za kimetali zenye namba atomia kutoka 57 hadi 71, ambazo tabia zake zinafanana. Elementi hizo huhesabiwa kati ya madini adimu kama vile monaziti. Kundi hilo huanza na lanthani na kuishia kwa luteti. [1] [2]

Lanthanidi ni metali zinazofanana katika tabia nyingi. Nyingi hubadilika polepole kuwa hidroksidi zake wakati zimewekwa ndani ya maji, sawa na metali alikali.

Hewani huunda kwa kawaida ganda jembamba la oksidi wakati sawa na metali nyingi. Lanthanidi, pamoja na Skandi na Ytri, huhesabiwa kati ya elementi za ardhi adimu. Lanthanidi zote ni metali nyeupe na laini zinazobadilisha rangi ya nje haraka zikiathiriana na hewa. Ugumu wake huongezeka sambamba na namba atomia.

Lanthanidi hazipatikani wala hazichimbwi kwa viwango vikubwa.

MatumiziEdit

Zina matumizi katika teknolojia mbalimbali kama vile:

*    Ceri: hutumiwa kama "jiwe la kibiriti" katika vibiriti vya gesi; pia kama kichocheo katika pirolisisi

*    Disprosi : hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia

*    Erbi : imo katika filta za kupiga picha

*    Europi : hutumiwa kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia, lakini pia kwa kuwasha rangi nyekundu katika skrini ya runinga

*    Gadolini : hutumiwa kuwasha rangi kibichi katika skrini ya runinga

*    Holmi : hutumiwa katika aloi; kwa jumla lanthanidi mbalimbali hutumiwa kama sehemu za aloi maana zinasaidia feleji kuwa nyumbufu zaidi wakati wa kuipa umbo

*    Luteti : kichocheo katika pirolisisi

*    Neodimi: huhitajika kwa sumaku kali; pia sehemu ya vioo vya miwani ya kinga cha mtia weko, hutumwa pia katika leza.

*    Praseodimi: katika kioo njano, k.v. kwa miwani ya kinga cha mtia weko.

*    Promethi : ikiwa ni nururifu hutumiwa kama chanzo cha nishati kwa satelaiti na vipimaanga

*    Samari : kama sumaku ya kudumu, mfano katika kipaza sauti

*    Terbi : kwa leza

*    Thuli : kufyonza nyutroni ndani ya tanuri nyuklia

*    Yterbi : hutoa eksirei ilhali haihitaji umeme, mfano katika mashine za eksirei za kubeba

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lanthanidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.