Leza
Leza (kutoka Kiingereza laser, akronimi ya fungu la maneno "Light Amplification by Stimulated Emission of Radiation"[1][2]) ni chombo cha kukuza na kushadidisha miali kuelekea upande mmoja kutengeneza mwangaza leza.
Kifaa hiki ni maalumu, si kama taa nyingine za kutoa mwangaza na miali yake ina matumizi mengi.
Historia
Leza ina historia kubwa na ni mojawapo wa nyanja zilizofanyiwa utafiti mkubwa tangu mwaka 1917. Utafiti wa leza umekua kutokana na utafiti wa mnururisho (radiation) na utafiti wa usumakuumeme (electromagnetism).
Manufaa ya leza
Leza ina matumizi mengi yakiwemo:
- Burudani - inatumika kwa vifaa vinavyosoma vijisahani rekodi (disc drives) na vifaa zinazotoa miali ya rangi tofautitofauti katika nyumba za burudani
- Biashara kwa vifaa kama vile vya kupiga chapa, vya kupima joto vya leza, vielekezi leza na vinginevyo
- Viwandani kutengeneza vifaa vya leza vya kukata, kuchomelea, kupima urefu kidijiti, kutia alama vitu na kuchomea vitu zinazoundwa kwa joto
- Mawasiliano - kupeperusha mawimbi ya runinga na intaneti[1]
- Usalama - katika ala za vita hasa tochi za kulenga shabaha katika vifaa vya kivita kama vile bunduki za kisasa, kuelekeza kombora za kisasa
- Matibabu - kufanya operesheni isiyo ya upasuaji[3]
- Upodozi - kufanya operesheni zisizo za upasuaji za kubadilisha umbile ili kuongeza urembo kama vile operesheni ya lipo ya leza (ijulikanayo kwa Kiingereza kama "Liposuction") inayopunguza mafuta mwilini. Operesheni ya lipo hufanywa na mashine ya lipo ya leza ambayo ilibatilisha mfumo wa zamani wa operesheni ya lipo ambao watu walifanyiwa upasuaji.
Tanbihi
- ↑ 1.0 1.1 NASA (25 Mei 2017). "What is a laser? :: NASA Space Place". spaceplace.nasa.gov (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-07-09.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Lawrence Livermore National Laboratory. "How Lasers Work". lasers.llnl.gov (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-07-09.
- ↑ Glaucoma Research Foundation (25 Agosti 2017). "Laser Surgery". Glaucoma Research Foundation (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-14. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser*
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_beam_quality
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_surgery
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_safety
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_printing
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_pointer
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_beam_welding
- https://en.wikipedia.org/wiki/Beam_riding
- https://en.wikipedia.org/wiki/LaserDisc
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_beam_machining
- https://en.wikipedia.org/wiki/Laser_beam_profiler
- https://en.wikipedia.org/wiki/Liposuction
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |