Lashinda Demus (alizaliwa 10 Machi 1983 mjini Inglewood, California) ni mwanariadha wa urukaji viunzi ambaye ni mtaalamu wa mbio ya 400m ya kuruka viunzi.

Lashinda Demus
Mwanariadha wa Marekani wa mbio za wanawake
Mashindano
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia
*Medali ya dhahabu - 2009 - Berlin - 4x400 m
*Medali ya fedha - 2005 - Helsinki - 400 m ya urukaji viunzi
*Medali ya fedha - 2009 - Berlin - 400 m ya urukaji viunzi

Muda wake bora wa kibinafsi katika mbio ya 400m ni 53.02s,aliohitimu katika mwezi wa Julai 2006 jijini Athens.

Yeye alikuwa katika Long Beach Wilson alipokimbia na bado anashikilia rekodi ya mbio ya 300m ya kuruka viunzi. Alikimbia pia mbio ya 4 x 400, 4 x 100 na ,vilevile, mbio fupifupi.

Lashinda Demus akishiriki katika mashindano ya Berlin katika mwaka wa 2009

Baada ya shule ya sekondari, Lashinda alihudhuria Chuo Kikuu cha Carolina Kusini kukimbia chini ya kocha Curtis Frye. Muda wake bora akiwa chuo kikuu:

  • mbio ya 55m ya urukaji viunzi: 7.80
  • mbio ya 60m ya urukaji viunzi: 8.32
  • mbio ya 100m ya urukaji viunzi: 13.35
  • mbio ya 400m ya urukaji viunzi : 54.70
  • mbio ya 400m: 51.38
  • mbio ya 800m: 2:13.77

Akitupilia mbali kumbukumbu za kushindwa hapo awali katika kuhitimu Olimpiki ya 2008 , alishinda Mashindano ya Mabingwa wa Marekani ya 2009 katika mbio ya 400m ya urukaji viunzi.Alishinda na muda wa sekunde 53.78 na kushinda nafasi ya kucheza katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2009. Aliboresha muda wake katika mbio za mashindano ya Herculis katika mwezi wa Julai ukawa sekunde 52.63. Hii ilikuwa rekodi katika mashindano hayo na muda wa kasi wa nne katika tukio hilo.

Mafanikio

hariri
Mwaka Mashindano Pahali pa kushindana Matokeo Maelezo ya ziada
2002 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya Vijana ya 2002 Kingston, Jamaica 1
2005 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2005 Helsinki, Finland 2
Mashindano ya Riadha ya IAAF Monte Carlo, Monaco 1
2006 Mashindano ya Riadha ya IAAF ya 2006 Stuttgart, Ujerumani 1
Mashindano ya Riadha ya IAAF ya Kombe la Dunia ya 2006 Athens, Ugiriki 2

Marejeo

hariri
  1. http://gamecocksonline.cstv.com/sports/c-track/mtt/demus_lashinda00.html Archived 6 Desemba 2009 at the Wayback Machine..
  2. Morse, Parker (2009-06-28). World season leads for Demus and Merritt as team takes shape in Eugene - USA Champs, Siku ya tatu. IAAF.
  3. Turner, Chris (2009-07-28). Hurdlers delight on a spectacular evening in Monaco - IAAF World Athletics Tour. IAAF.

Viungo vya nje

hariri