Leodegar wa Autun (kwa Kilatini: Leodegarius; kwa Kifaransa: Léger; Autun, Saône-et-Loire, 615 hivi – Sarcing, Somme, Picardie, 2 Oktoba 679) alikuwa askofu wa Autun, mtoto wa mtakatifu Sigrada na ndugu wa mtakatifu Warinus[1][2].

Kifodini cha Mt. Leger. Mchoro mdogo wa mwaka 1200 hivi unaonyesha alivyotobolewa macho.

Kwa kuwa alimpinga Ebroin aliyetaka kupindua utawala wa ukoo wa Wamerovinji aliteswa na kuuawa[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3]. Pamoja naye anaheshimiwa ndugu yake Warinus aliyeuawa miaka miwili kabla yake[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 Butler, Rev. Alban. The Lives of the Saints, Volume X: October.. St. Leodegarius, or Leger, Bishop and Martyr. bartleby.com. Iliwekwa mnamo June 28, 2012.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90609
  3. Martyrologium Romanum
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90284

Vyanzo hariri

Vyanzo vikuu hariri

  • Liber Historiae Francorum, edited by B. Krusch, in MGH SS rer. Merov. vol. ii.
  • Passio Leudegarii I & II, edited by B. Krusch and W. Levison, in MGH SS rer. Merov. vol v.
  • Vita sancti Leodegarii, by Ursinus, then a monk of St Maixent (Migne, Patrilogia Latina, vol. xcvi.)
  • Vita metrica in Poetae Latini aevi Carolini, vol. iii. (Mod. Germ. Hist.)
  • Epistolae aevi Merovingici collectae 17, edited by W. Gundlach, in MGH EE vol iii.

Vyanzo vingine hariri

  • J. Friedrich, Zur Geschichte des Hausmeiers Ebroin, in the Proceedings of the Academy of Munich (1887, pp. 42–61)
  • J. B. Pitra, Histoire de Saint Léger (Paris, 1846)

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.