Leonida, Karisa na wenzao

Leonida, Karisa na wenzao Galinia, Theodora, Nike, Nunesia, Kalide na Basilisa (walifariki Korintho, 258 hivi[1]) ni kati ya Wakristo wa Ugiriki ambao waliteswa kwa namna mbalimbali na hatimaye kuuawa kwa kutoswa baharini kwa ajili ya imani yao wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[2].

Tangu kale huyo mwanamume na hao wanawake saba wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini. Pengine anaongezwa pia Irene.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Aprili[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.