Leto wa Nefta (alifia dini 483), alikuwa askofu wa mji huo (leo nchini Tunisia) na ni kati ya wafiadini wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario.

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Mtu mwenye ujuzi na msimamo, alifungwa muda mrefu na hatimaye alichomwa moto ili kutisha maaskofu Wakatoliki wenzake.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Septemba[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.