Lualaba (mto)
(Elekezwa kutoka Lualaba)
Lualaba ni tawimto kubwa la Mto Kongo yaani inabeba maji mengi kuliko matawimto mengine. Inawezekana pia kusema ni jina la mto Kongo juu ya Maporomoko ya Boyoma karibu na mji wa Lubumbashi.
Lualaba ni mto uliopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Urefu wa mwendo wake ni kilomita 1,800. Vyanzo vyake viko katika sehemu za Katanga karibu na Zambia.
Tawimto lake refu zaidi ni mto Chambeshi unaoanza nchini Zambia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lualaba (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |