Lucky Isibor
Anthony Joseph "Lucky" Isibor (1 Januari 1977 – 24 Juni 2013) alikuwa mcheza mpira wa Nigeria.[1]
Fani
haririAnthony alikuwa akicheza mpira katika timu ya Concord FC ya nchini Nigeria,mwaka 1995 alihamia nchini Switzerland na kuingia mkataba wa kuichezea timu ya AC Bellinzona, kati ya mwaka 1996 na 1998 aliichezea timu ya FC Koper[2] na timu ya Enosis Neon Paralimni FC kabla ya kuingia mkataba na timu ya A.C. Reggiana 1919 ya nchini Italia; baadae alihamia nchi ya Urusi na kuchezea timu ya FC Dynamo Moscow ambayo ilikuwa ikishiriki ligi kuu mwaka 1998.[3] , baada ya hapo alienda nchini Korea Kusini na kuchezea timu ya Suwon Samsung Bluewings, timu ya FC Zürich ilikataa kuendelea na mkataba wake baada ya kugundua Anthony ni muathitika wa virusi vya Ukimwi lakini baadae mahakama iliilazimisha timu hiyo kulipa kiasi cha fedha za Kiswizi 31500 kwa madai kwamba Ukimwi haukuwa sababu ya wao kusitisha mkataba na Anthoni Joseph.
Kifo
haririAnthony alifariki tarehe 24 Juni 2013 katika jiji la Lagos baada ya kuumwa kwa muda mrefu .[4]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lucky Isibor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |