Lukio wa Kurene (kwa Kigiriki Λούκιος ὁ Κυρηναῖος, Loukios o Kurenaios) kadiri ya Matendo ya Mitume 13ː1 alikuwa nabii na kiongozi mmojawapo wa Kanisa la kwanza huko Antiokia, jiji la Syria katika Dola la Roma (leo nchini Uturuki)[1].

Kwa kuzingatia dondoo lingine la Luka mwinjili (Mdo 11ː19-20) inafikiriwa alikuwa kati ya Wakristo wa kwanza waliochukua jukumu la kuwapasha watu wa mataifa habari njema ya Yesu Kristo.

Anatajwa pia kama askofu wa kwanza wa Kurene, mji wake wa asili, uliokuweko Libya mashariki.[2]

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 6 Mei[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/52050
  2. Walsh, Michael J., (2007) A New Dictionary of Saints: East and West p. 372
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo hariri

  • Walsh, Michael A New Dictionary of Saints: East and West London: Burns & Oats 2007 ISBN 0-86012-438-X

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lukio wa Kurene kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.