Lupo wa Sistov (alifariki Sistov, leo nchini Bulgaria, 307 hivi) alikuwa mtumwa aliyefia imani ya Kikristo hukohuko kwa kuchomwa kwa upanga[1], kama alivyofia dini bwana wake Dimitri wa Thesalonike, wakati wa dhuluma ya kaisari Galerius wa Dola la Roma.

Mchoro wa ukutani wa karne XVIII ukimuonyesha Mt. Lupo.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Agosti[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.