Lupus wa Sens (au Loup wa Sens) (573 hivi - 623 hivi)[1] alikuwa askofu wa 19 wa Sens, Ufaransa.

Mt. Lupus wa Sens akigawa sadaka; mchoro mdogo wa karne ya 14.

Alikuwa mtoto wa Betton, kabaila wa Tonnerre, kutoka ukoo uliotawala Burgundy.[1] Kwa ushujaa wake alipelekwa uhamishoni[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba[3][4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: