Lutgarda (pia: Lutgardis, Lutgarde, Ludgardis, Lutgard, Luitgard, Ludgard, Lutgart au Luthgard; Tongeren, leo nchini Ubelgiji, 1182 hivi – Aywières, leo nchini Ubelgiji, 16 Juni 1246) alikuwa bikira aliyejiunga na monasteri ya Kibenedikto bila wito akiwa na miaka 12[1].

Mt. Lutgarda alivyochorwa na Goya, 1787.

Miaka 8 baadaye alipata njozi iliyomfanya achangamkie maisha ya kiroho[2].

Baadaye tena alihamia urekebisho wa Citeaux akazidi kujaliwa karama za pekee[3][4].

Miaka 11 ya mwisho ya maisha yake alibaki kipofu.

Inakumbukwa ibada yake ya pekee kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[5].

Anaheshimiwa tangu zamani kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[6].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Thomas Merton, The Life of a Cistercian Mystic: Saint Lutgarde of Aywières (Milwaukee: Bruce Publishing Company, 1950)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.