Rubela (inajulikana pia kama surua ya Kijerumani au surua ya siku tatu) [1] ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya rubela. Ugonjwa huu mara nyingi si mkali na nusu ya watu hawajitambui kuwa ni wagonjwa.[2]

Mtoto anayeonyesha dalili za rubela ya kuzaliwa nayo.

Upele unaweza kuanza karibu wiki mbili baada ya kushambuliwa na hivyo virusi na hudumu kwa siku tatu. Kawaida huanza kwenye uso na kuenea kwa mwili wote. Upele si mkali kama ule wa ukambi na wakati mwingine huwa mkali. Homa, maumivu ya koo, na uchovu huweza pia kutokea. Maumivu ya viungo kwa watu wazima ni kawaida. Dalili nyingine ni pamoja na za kutokwa na damu, uvimbe wa pumbu, na kuvimba kwa mishipa. Kuambukizwa mwanzoni mwa ujauzito kunaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na ugonjwa huu au kuharibika mimba.

Rubela kawaida huenea kupitia hewani kwa kikohozi cha watu ambao wameambukizwa.[3] Watu wanaambukiza wiki kabla na baada ya kuonekana kwa upele. Watoto wanaweza kueneza virusi kwa zaidi ya mwaka. Wanadamu tu ndio wanaoambukizwa. Wadudu hawaenezi ugonjwa. Watu wanapopona hawaambukizwi tena. Upimaji unapatikana ambao unaweza kudhibitisha kinga. Utambuzi unathibitishwa kwa kupata virusi kwenye damu, koo, au mkojo.

Rubela inaweza kuepukwa kwa kutumia chanjo ya rubella iliyo na kipimo kizuri cha kinga zaidi ya asilimia 95. Mara nyingi hupewa pamoja na chanjo ya ukambi na matumbwitumbwi. Wakati baadhi ya watu, lakini idadi ya watu chini ya asilimia 80, wamepatiwa chanjo, wanawake wengi wanaweza kufikia umri wa kuzaa na bila kuwa na kinga kutokana na chanjo au baada ya kuambukizwa. Ikitokea wakaambukizwa hakuna matibabu maalum.[4]

Maambukizi ya rubela ni kawaida katika maeneo mengi ya ulimwengu. Kila mwaka takriban kesi 100,000 za ugonjwa huu hujitokea.[5] Viwango vya magonjwa vimepungua katika maeneo mengi yakiwa ni pamoja na Amerika kwa sababu ya chanjo. Kuna juhudi zinazoendelea kumaliza ugonjwa huu ulimwenguni.

Jina "rubella" ni la Kilatini na linamaanisha nyekundu nyekundu. Ilielezewa kwanza kama ugonjwa tofauti na waganga wa Ujerumani mnamo 1814 na kusababisha jina la surua ya Kijerumani.[6] --> It was first described as a separate disease by German physicians in 1814 resulting in the name German measles.[6]

Marejeo hariri

  1. Neighbors, M; Tannehill-Jones, R (2010). "Childhood diseases and disorders". Human diseases (toleo la 3rd). Clifton Park, New York: Delmar, Cengage Learning. ku. 457–79. ISBN 978-1-4354-2751-8. 
  2. "Rubella vaccines: WHO position paper.". Wkly Epidemiol Rec 86 (29): 301–16. 15 July 2011. PMID 21766537.  Check date values in: |date= (help)
  3. "Rubella (German Measles, Three-Day Measles)". cdc.gov. December 17, 2014. Iliwekwa mnamo 30 March 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. Huong McLean (2014). "3 Infectious Diseases Related To Travel". CDC health information for international travel 2014 : the yellow book. ISBN 9780199948499. 
  5. Lambert, N; Strebel, P; Orenstein, W; Icenogle, J; Poland, GA (7 January 2015). "Rubella.". Lancet. PMID 25576992.  Check date values in: |date= (help)
  6. 6.0 6.1 Atkinson, William (2011). Epidemiology and Prevention of Vaccine-Preventable Diseases (toleo la 12). Public Health Foundation. ku. 301–323. ISBN 9780983263135. Iliwekwa mnamo Mar 2015. 
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rubela kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.