Maambukizi nyemelezi

Maambukizi nyemelezi (pia: maradhi nyemelezi, magonjwa nyemelezi; kwa Kiingereza: opportunistic infections) ni magonjwa ya kuambukizwa ambayo yanaweza kutokea wakati ugonjwa mwingine umeshadhoofisha mfumo wa kinga mwilini wa binadamu. Katika hali hiyo bakteria, fungi, virusi na vimelea - ambavyo kwa hali ya afya ya kawaida vinazuiliwa na mfumo wa kinga - vinapata nafasi kusambaa mwilini na kusababisha magonjwa.

Maambukizi nyemelezi ambayo unaweza kuyapata baada ya kuambukizwa ugonjwa wa ukimwi, ni kutokwa na jasho usiku, kutokwa na vipele mwilini au ukurutu, kuwashwa sehemu za mikononi na miguuni, kuharisha mfululizo zaidi ya mwezi mmoja, kutapika, kutokwa na tezi sehemu za shingoni, kuishiwa nguvu mwilini, kutokwa na mafua, kukosa hamu ya kula, maumivu makali kiunoni au mgongoni na kupelekea kuathiri akili, kupotea kwa kumbukumbu, kuambatana pamoja na kifua kikuu, kuumwa na tumbo, kupungua uzito zaidi ya asilimia kumi.

Hizo dalili hutokea baada ya miezi mitatu, na si kila dalili uipatayo kati ya hizo una ukimwi, ila ni vyema kwenda hospitali kucheki mwili wako sababu dalili hizo hutokea na kupotea sababu virusi vya ukimwi huwa vinapambana na kinga mwilini, baada ya kinga kushindwa, magonjwa nyemelezi ya hapo juu yanaanza kujitokeza upya; ni vyema kwenda kupima hospitalini na kupata ushauri wa daktari na jambo tu la kukumbushia ugonjwa huo hauna dawa wala chanjo, ni janga kubwa kwa dunia nzima na gharama zake ni kubwa mno.

Kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa hup ni vyema kuanza dozi au kutumia dozi ipasavyo kwa muda mwafaka kwa sababu ugonjwa huo ukiacha tu kutumia dozi virusi hivyo vinazidi tena kwa kasi na dozi hiyo haiponeshi bali inafanya virusi vya HIV walewe ili wasiendelee kuongezeka na hivyo inaupa mwili nguvu.

Tovuti za nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maambukizi nyemelezi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.