Madina (pia: Medina; Kiarabu: المدينة المنورة madinat-ul-munawwara - mji ulioangazwa) ni mji wa Saudia ya magharibi takriban 320 km kaskazini ya Makka. Inaheshimiwa na kutembelewa na Waislamu kwa sababu ni mahali pa kuzikwa kwa Mtume Muhammad.

Faili:Masjid Nabawi. Medina, Saudi Arabia.jpg
Masjid an-Nabawi (Msikiti wa Mtume) mjini Madina.
Mahali pa Madina

Madina ina wakazi mnamo 900,000. Jina asilia ya mji lilikuwa Yathrib. Neno "madina" lamaanisha "mji".

Madina ina nafasi muhimu katika imani ya Kiislamu. Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu Muhammad alifika hapa mwaka 622 kwa njia ya hijra alipoondoka Makka kwa sababu ya upinzani dhidi yake.

Yathrib alipokelewa vizuri na kuwa kiongozi wa kisiasa pamoja na kiongozi wa kiroho. Jina la "madinat-un-Nabii" (mji wa Mtume) lilianza kutumiwa.

Kwa kawaida huhesabiwa kuwa mji mtakatifu wa pili katika Uislamu baada ya Makka. Hapa kuna msikiti wa Mtume penye kaburi la Muhammad kwenye mahali panapoaminiwa ni mahali pa nyumba yake alikoaga dunia. Kando lake kuna makaburi ya wenzake Muhammad.

Mji huu ni marufuku kwa wasio Waislamu wasiingie sawa na Makka.