Hijra
Hijra (هجرة) ni neno la Kiarabu linalomaanisha tendo la Mtume Muhammad la kutoka Makka na kuhamia Madina mwaka 622 BK. Mwaka huo umekuwa tarehe ya kuanzisha kalenda ya Kiislamu ambayo miaka yake huhesabu miaka baada ya hijra.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Maana asili ya neno lenyewe ni "kuachana" au "kutengana", kutokana na historia ya Muhammad limechukua pia maana ya "kukimbilia" au "kuhamia".
Historia ya Hijra
haririMuhammad alianza kuhubiri habari za Qurani na za Uislamu katika mji wa Makka alipozaliwa na kuishi. Lakini hakupata wafuasi wengi. Kinyume chake kabila lake yeye mwenyewe la Waquraishi walimchukia na kumtesa kwani viongozi waliogopa ataharibu biashara kubwa iliyoletwa na Kaaba iliyokuwa kama hekalu ya kidini mjini.
Hivyo Muhammad aliondoka Makka pamoja na babake mkubwa Abu Bakr; wafuasi wake kama 70 waliwahi kuondoka Makka siku zilizotangulia. Wote walipokelewa na watu wa Madina mji wa jirani.
Hapo Madina Muhammad akawa kiongozi aliyekubaliwa na watu wengi katika miaka iliyofuata aliunganisha Waarabu katika Uislamu mwishowe akarudi Makka ambako Waquraishi walipaswa kumkubali yeye na dini ya Usilamu.
Katika kumbukumbu ya Waislamu wa kwanza tendo la hijra lilikuwa jambo muhimu sana. Sura za Qurani zilipokusanywa kila moja imeandikwa kama imepatikana kabla au baada ya hijra. Kila sura inaonyesha chini ya kichwa chake maneno ama (imeteremka Makka) au (imeteremka Madina).
Pia hesabu ya miaka ilianzishwa wakati wa khalifa wa pili Umar ikihesabu kuanzia tarehe ile ya kuhamia kwake Muhammad Madina.