Maghofu ya Ras Mkumbuu

Eneo la Kihistoria la Taifa la Tanzania

5°13′00″S 39°40′00″E / 5.21667°S 39.66667°E / -5.21667; 39.66667

Mahali pa Ras Mkumbuu kwqenye kisiwa cha Pemba

Maghofu ya Ras Mkumbuu yanapatikana kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa cha Pemba (Tanzania). Yapo karibu na kijiji cha Ndagoni mwishoni mwa rasi ndefu nyembamba inayojulikana kama Ras Mkumbuu iliyopo upande wa kaskazini magharibi mwa mji wa Chake Chake.

Kutokana na utafiti wa kiakiolojia maghofu yanatokana katika kipindi cha karne ya 13 na 14, ingawa kuna dalili kwamba yalijengwa juu ya misingi ya kale zaidi. Miongoni mwa maghofu haya kuna msikiti mkubwa.

Mwanaakiolojia James Kirkman aliyekuwa wa kwanza kuchimba hapa katika miaka ya 1950, alipendekeza kuona maghofu haya ni mabaki ya "Qanbalu" (pia: Kanbalu, kwa Kiarabu: قنبلاو) iliyotajwa na mpelelezi Mwarabu Al-Masudi mnamo mwaka 900 BK[1] lakini hakuweza kutambua mabaki ya zamani kuliko karne ya 13 [2] .

Wataalamu bado wanajadiliana kama "Qanbalu" ya Al Masudi ilikuwa kisiwa cha Pemba kwa ujumla na labda hasa mahali pa maghofu ya Ras Mkumbuu [3] .

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Al-Masudi: Meadows of Gold and Mines of Gems, an English translation of the Muruj al-dhahab by Aloys Sprenger, London 1841 (google books), uk. 232,260
  2. Reid, Lane: African Historical Archaeologies (2014) (kupitia google books), p. 135f
  3. Oliver, Oliver & Fagan: Africa in the Iron Age: C.500 BC-1400 AD (1975) (kupitia google books) , p. 193f Hao wanasema ya kwamba Ras Mkumbuu imethibitishwa kuwa sawa na Qanbalu, lakini wengine hawakubali

Marejeo

hariri
  • Finke, J. (2006) The Rough Guide to Zanzibar (2nd edition). New York: Rough Guides.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Pemba bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maghofu ya Ras Mkumbuu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.