Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya Tanzania

orodha ya Maeneo ya Urithi wa Taifa wa Tanzania

Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya Tanzania ni orodha kuu rasmi ya maeneo mbalimbali nchini Tanzania ambayo yameteuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania chini katika Kitengo cha Mambo ya Kale. [1] Orodha hii haijakamilika na inafanyiwa kazi kwa sasa.

Eneo la Zama za Mawe huko Ismila, Iringa.

Historia

hariri

Historia ya Idara ya Mambo ya Kale na Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa iliundwa na mamlaka ya Waingereza katika eneo la Tanganyika mwaka 1937 kama Sheria ya Uhifadhi wa Maziara ya mwaka wa 1937. Ilipofika mwaka wa 1957, idara hiyo ilikabidhiwa kwa Wizara ya Elimu kama Kitengo cha Mambo ya Kale kilichozinduliwa na ofisi iliyopo Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Ofisi ilihamishiwa rasmi kwenda Dar es Salaam mwaka 1960. Ulipofikia mwaka wa 1964, miaka mitatu baada ya uhuru wa taifa, Bunge la taifa la Tanzania lilipitisha Sheria ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 ili kuchukua nafasi ya Sheria ya Uhifadhi wa Makumbusho ya 1937. [2] Sheria ya 1964 ilirekebishwa mwaka wa 1979 na kuwekwa kwa Sheria ya Mambo ya Kale Na. 22 ya mwaka 1979, kisha hiyo nayo ikabadilishwa na Sheria ya Makumbusho ya Vitu Na. 13 ya mwaka 1981 ambao ndiyo sheria iliyomo mpaka leo. [3]

Orodha ya Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa

hariri

Ifuatayo hapo chini ni orodha ya Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya nchi ya Tanzania. [4] Kuna vituo vya ziada kwa mikoa kwenye hii orodha. [5]

  • Bombo Kaburi (Makazi ya Zama za Chuma)
  • Marangu (Mapango ya kujihami, karne ya 19)
  • Pare (Makazi ya Zama za Chuma)
  • Usangi (Makazi ya Zama za Chuma)
  • Tumbatu ((Makazi ya Waswahili wa Zama za Kati)

Uongozi na Wizara

hariri

Ifuatayo ni historia ya idara ya mambo ya kale nchini Tanzania; imekuwa chini ya uongozi wa watu wafuatao: [6]

*1957-1968: Neville Chittick, Mtunza

*1968-1981: Amin Aza Mutri, Mkurugenzi

*1981-1985: Simon S.A. Waane, Mkuu wa Sehemu

*1985-1997: Simon SA Waane, Mkurugenzi

*1997-2000: Donatius M.K. Kamamba, Ag Mkurugenzi

*2000-Hadi sasa: Donantius M.K. Kamamba, Mkurugenzi


Idara ya Mambo ya Kale ya Tanzania imekuwa chini ya wizara zifuatazo:

*1957-1962: Wizara ya Elimu

*1962-1964: Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana

*1964-1967: Ofisi ya Rais 1967-1968: Wizara ya Tawala za Mikoa *1968-1980: Wizara ya Elimu ya Taifa

*1980 -1984: Wizara ya Habari na Utamaduni

*1984-1999: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Utamaduni, Vijana na Michezo

*1999–Sasa: Wizara ya Maliasili na Utalii.

Tanbihi

hariri
  1. https://www.maliasili.go.tz/sectors/category/antiquities
  2. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-11-03. Iliwekwa mnamo 2021-12-22.
  3. http://www.parliament.go.tz/polis/uploads/bills/acts/1566374555-The%20Antiquities%20(Amendment)%20Act,%201979.pdf
  4. https://www.maliasili.go.tz/uploads/ANTIQUITIES_SITES_LOCATION_AND_ACCESSBILITY.pdf
  5. https://www.nps.gov/CRMJournal/winter2010/article1.html
  6. https://www.maliasili.go.tz/sectors/category/antiquities