Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa (kwa Kiingereza: African Court on Human and Peoples' Rights) ni mahakama ya kibara iliyoanzishwa na nchi za Afrika ili kulinda haki za binadamu na za mataifa barani humo.[1]

African Union

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
the African Union



Nchi zingine · Atlasi
Nchi wanachama wa African Court on Human and Peoples' Rights.
Pinki iliyokolea - nchi zinazokubali mamlaka ya mahakama hiyo
Pinki - nchi nyingine zilizosaini hati ya kuunda mahakama hiyo.

Uamuzi huo ulichukuliwa na OAU huko Ouagadougou, Burkina Faso, mnamo Juni 1998 ukapata nguvu ya kisheria tarehe 25 Januari 2004 baada ya nchi 15 kuupitisha kwa saini (kwa sasa zimekuwa 30[2]).

Mahakama inaundwa na mahakimu 11, wote raia wa nchi za Umoja wa Afrika. Wale wa kwanza walianza kazi yao mwaka 2006 huko Addis Ababa, Ethiopia lakini mnamo Agosti 2007 mahakama ilihamia Arusha, Tanzania.

Tanbihi hariri

  1. Kate Stone, African Court of Human and People's Rights (Advocates for International Development, February 2012). Legal Guide (2012)
  2. Algeria, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d'Ivoire, Comoros, Republic of the Congo, Gabon, Gambia, Ghana, Kenya, Libya, Lesotho, Mali, Malawi, Mozambique, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Sahrawi Arab Democratic Republic, South Africa, Senegal, Tanzania, Togo, Tunisia, and Uganda.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na za Mataifa kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.