Majadiliano:Jumuiya ya Afrika Mashariki

Latest comment: miaka 15 iliyopita by Muddyb Blast Producer

Makala nzuri sana - na nimeisawazisha vilivyo. Sasa imekuwa makala halisi. Ongezeko linakaribishwa. Lakini uharabu? Hapana! Basi endelea ndugu uliyeanzisha makala hii.--Muddyb MwanaharakatiLonga 11:45, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply

Ndugu uliyeanzisha makala hii - unaombwa usifute haya yaliyowekwa sasa hivi hata kama wewe ndiye uliyenzisha. Umeanzisha, nikaboresha na kuiweka katika viwango vya wiki, lakini cha kushangaza umerejesha lile toleo lako la awali. Hii siyo nzuri. Tafadhali usiendelee kufanya hivyo.--Muddyb MwanaharakatiLonga 11:54, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply
Naona ametambua ya kwamba makala Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iko tayari. Naona ilikuwa sawa kufuta ingawa kama makala ya awali isingekuwepo hiyo hapa ingefaa. --Kipala (majadiliano) 12:30, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply
Hapana mzee wangu. Sijajua kama makala hii awali ilikuwepo! Lakini ile ya zamani haina maelezo marefu kama hii ya sasa. Sijui la kuamua. Tuifanyaje hii?--Muddyb MwanaharakatiLonga 15:24, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply
Angalia historia. Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ilianzishwa 4 Februari 2006. Urefu pekee si ubora. Maana wageni wetu wa mashindano mara nyingi hupitisha makala ya Kiingereza kwenye google translation tool; wengine hawajitahidi hata kidogo, wengine kiasi, wachache wanajitahidi kuswahilisha kweli. Je unaelewa wewe sentensi ya pili: "Wakati kwa ujumla, mataifa wanachama kwa kiasi kikubwa ni katika neema ya Shirikisho la Afrika Mashariki uchaguzi usio rasmi unaonyesha kwamba Watanzania wengi (asilimia themanini (80%) ya wakazi wake) wana mtazamo wa kinyume" ???
Naona vema amefuta mwenyewe. Ukipenda unaweza kuunganisha makala ukiona habari za nyongeza za uhimu. --Kipala (majadiliano) 21:23, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply
Kweli kabisa Wabongo hatuungi mkono hoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, lakini viongozi walifosi. Shida hasa ilikuwa elimu ya Bongo bado iko nyuma kiasi kwamba Wabongo tuliowengi hatuna elimu ya kutosha. Hivyo, kupelekea tumbo joto kwa wananchi na hata maprofesa walijaribu kulizungumzia hilo. Alichoeleza kuhusu ardhi, hapana, Wabongo hawaku hofia ardhi yao, bali ajira zao! Mengine niliyosikia ilikuwa suala la ubaguzi, wengi walidai kwamba Kenya, Rwanda, Burundi wenyewe kwa wenyewe wanabaguana - je itakuwaje wakina sisi? Basi imeishia hivyo-hivyo na wakubwa washaamua... Nasema shaurilao wenyewe!!! Kuhusu ubora, kweli ya sasa imekosa maelezo ya maana sana. Hivyo kazi kwako.--Muddyb MwanaharakatiLonga 07:09, 5 Desemba 2009 (UTC)Reply
Rudi kwenye ukurasa wa " Jumuiya ya Afrika Mashariki ".