Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Tangazo

hariri
Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 20:13, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Uteuzi kuwa mkabidhi

hariri

Salaam! Ulipendekezwa na kukubaliwa kupata haki za mkabidhi. Je, uko tayari kupokea uteuzi huu na kushiriki katika kazi mara kwa mara kama jinsi ilivyoelezwa katika ukurasa wa wakabidhi? Tunaomba jibu lako kwa baruapepe katika wiki hii. Tumia zana za Wikipedia kutuma barua pepe. --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 07:46, 13 Septemba 2020 (UTC) Reply

Mfano wa makala ya kata

hariri

Kwa jumla hongera, umeshika mfumo haraka na vizuri. Nadhani ni zoezi nyepesi; angalia tu kama majina mekundu yanatosha (kwa kufungua wilaya zote za mikoa Dodoma, Arusha, Morogoro na kukadiria idadi), kwa sababu ni vizuri kama kila mmoja anaweza kurudia kazi mara kadhaa. Kuna mawili:

  1. Nilifanya kosa dogo kwa kuingiza [[Jamii:Wilaya za Mkoa wa Morogoro]] ambayo haina maana kwenye makala za kata (inahitajika kwenye makala za wilaya). Nimesahihisha na kuiondoa.
  1. Kabla ya kuhifadhai angalia yote kwa kubofya "Onyesha hakikisho la mabadiliko" uangalie kama jamii chini bado ni nyekundu. Katika majaribio yako ulitumia "Jamii:Wilaya ya Dodoma mjini" inayoonekana nyekundu maana jina ni kwa "M" kubwa yaani "Jamii:Wilaya ya Dodoma Mjini". Hi ni tatizo dogo kwa sababu wachangiaji mbalimbali walianzisha jamii kwa tahajia tofauti kidogo. Inafaa tuangalie ile preview hadi chini. Kipala (majadiliano) 15:10, 28 Septemba 2020 (UTC)Reply

Masahihisho ya Chalinze

hariri

Kazi nyingine nyepesi: tafadhali uweke watu 2 kwenye kata za Chalinze. Karibu zote bado zinasema ni kata za Bagamoyo. Wafungue zote kwa rightclick kando-kando (hariri chanzo) na kusahihisha ifuatayo:

Nimeandaa kata ya kwanza Bwilingu. Hatua ni mbili:

A) Wafungue Bwilingu na kukopi sehemu kuanzia Marejeo kwenda chini. Hii wanaweza kumwaga kwenye kila makala badala ya sehemu iliyopo sasa na kuonyesha Bagamoyo.

B) Wasahihishe kwenye mstari wa kwanza "Wilaya ya Bagamoyo" iwe Wilaya ya Chalinze. Kipala (majadiliano) 20:26, 28 Septemba 2020 (UTC)Reply

Kundi la Whatsapp

hariri

Habari tumeanzsha kundi la whatsapp kwa wakabidhi.Ukiwa na whatsapp, tafadhali nitumie namba yako. Kipala (majadiliano) 17:32, 1 Desemba 2020 (UTC)Reply

Makala za viumbe hai

hariri

Aneth, habari yako? Tuzungumze kuhusu makala za viumbe hai. Unaweza kuniuliza swali lolote unalopenda. Kuhusu sanduku la uainishaji, fungua Kigezo:Uainishaji (Mimea) ili kuona majina ya taksoni kadhaa. Kila la heri. ChriKo (majadiliano) 14:38, 26 Februari 2021 (UTC)Reply

Nashukuru sana kwa msaada kuhusu makala za viumbe hai. Mimi ni mwanabiolojia/bioteknolojia niliyebobea zaidi kwenye kilimo, hivyo nina ujuzi kwenye mimea zaidi na wadudu kwa kiasi. Kwa sasa ninatafsiri makala hii List of Orchidaceae genera kwenda Orodha ya jenasi za Orchidaceae. Swali la kwanza, kuna sehemu nakuta jina la jenasi linafuatiliwa na jina lingine (common name) kwa kingereza, nimetoa common names zote kwenye makala ya kiswahili kwa kuhofia kunaweza kua na common name nyinginge ambayo tunaita sisi. Hili ni sawa?
Hi Aneth. Hakuna haja ya kuandika majibu yako kwa majumbe yangu kwenye ukurasa wangu wa majadiliano. Ukurasa wako uko katika orodha yangu ya zile ninazofuata. Ni sawa kwamba umeondoa majina ya kienyeji ya Kiingereza kwenye orodha ya Kiswahili. Walakini, niliona kuwa umeacha jina moja la kienyeji. Vanila labda ni jina linalotumiwa zaidi kwa spishi hii siku hizi. Lakini ulijua kuwa zamani lavani lilitumika sana? Kwa ukweli, inaonekana kama lilikuwa jina la kwanza kutumika kwa Kiswahili.
Nashukuru kwa ujumbe, bado najifunza kutumia platform za wikipedia ya kiingerez na kiswahili ikiwemo kutumia kurasa za majadiliano.

Vanilla sikua na uhakika sana nikaiacha ila ni vzuri nimejua jina sahihi ni lavani, nitabadilisha hivi punde. Natumai watu wengine wenye uzoefu zaidi na okidi wataongeza majina ya kienyeji. Aneth David (SLU) (majadiliano) 12:21, 28 Februari 2021 (UTC)Reply

Sasa utafanyaje? Utatafsiri makala za okidi yote? ChriKo (majadiliano) 10:40, 27 Februari 2021 (UTC)Reply
Yani natamani ningeweza kufanya hivi, nimevutiwa sana na jenasi za okidi na kuna kitabu nasoma ndio kinanipa hamasa zaidi. Kwa hiyo nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuendelea kuandika na kutafsiri makala za okidi zaidi.

Ila pia nimejiunga kwenye project ya Wikipedia in Red sababu napenda kuchangia makala za wanawake hasa watanzania, nitatafuta namna ya kubalance muda niweke kidogo huku na kwenye makala za okidiAneth David (SLU) (majadiliano) 12:21, 28 Februari 2021 (UTC)Reply

Hongera

hariri

Napenda kukupongeza kwa juhudi zako katika Wikipedia, ila hakikisha kwamba makala zako zieleweke kwa Kiswahili. Unavyojua, tafsiri ya kompyuta haisaidii sana. Endelea kuangalia kama pengine ninarekebisha michango yako ili uzidi kukomaa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:37, 16 Aprili 2021 (UTC)Reply

Nashukuru sana Riccardo! Kusema kweli napata changamoto kuandika makala kwa kiswahili japo ni mzungumzaji mzawa. Hua naandika na kutafsiri kadri ya uwezo wangu na kutumai watu wengine watanirekebisha. Hua siachi tafsiri ya computer peke yake. Naendelea kujifunza Aneth David (SLU) (majadiliano) 11:52, 16 Aprili 2021 (UTC)Reply
Hongera kwa ukurasa wako juu ya Siku ya DNA! Penye nia pana njia! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:02, 23 Aprili 2021 (UTC)Reply
Nahsukuru sana! Nimepata msaada kwa wanafunzi wangu ambao pia wanajifunza kuhariri Wikipedia. They made the initial translation then tukaupload pamoja nikamalizia na marekebisho ya hapa na pale kama vyanzo vya ndani. Ila pia nina swali, kwenye makala ya kiingereza ya DNA day kuna info box ya holiday, ambayo nikiweka kwenye makala ya kiswahili haitokei. Je, kuna infobox ya sikukuu kwenye wikipedia ya Kiswahili?
Mimi sijawahi kuiona, labda kwa sababu situmii infobox!!! Kwangu ni ngumu mno... Jaribu kumshirikisha Muddy au Kipala, wataalamu wetu. Amani kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:59, 24 Aprili 2021 (UTC)Reply
Sawa. Ngoja niwaulize wengine. Nimeshatumia infobox kadhaa ila bado najifunza pia, hasa za kiswahili

Kigezo cha Vyanzo

hariri

Siku hizi unaweka mara kadhaa kigezo hicho. Badala ya kuridhika kuweka vigezo vinavyoagiza kazi fulani, tunashauriwa kufanya wenyewe kazi hiyo, yaani tuboreshe makala, si kuilaumu tu. Pia zingatia kwamba makala nyingi za zamani hazina vyanzo kwa sababu ya kutovisisitiza mwanzoni mwa Wiki yetu. Hatimaye makala nyingine haziwezi kuwa ndefu wala kuwa na vyanzo vingi kutokana na mada yenyewe, k.mf. Pagieli. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:38, 21 Aprili 2021 (UTC)Reply

Habari Riccardo!

Ndiyo niliweka kigezo hicho kwenye makala kadhaa ambazo hazikua na chanzo hata kimoja. Mara nyingi nikipitia mabadiliko ya hivi karibuni hua sina nafasi ya kufanyia marekebisho makala zote zenye walakini, hivyo kama kitu kinachokosena na chanzo, naweka kigezo kama hicho.

Naelewa kwamba kuna makala nyingine ni fupi na haziwezi kurefuka, ila ni sawa kua na makala isiyo na chanzo hata kimoja? Mfano makala ya Pagieli, biblia haiwezi kua chanzo? Asante Aneth David (SLU) (majadiliano) 15:22, 23 Aprili 2021 (UTC)Reply

Makaribisho

hariri

Samahani, naona umeweka kigezo cha karibu katika kurasa za watumiaji, kumbe mahali pake ni katika majadiliano yao, na huko tayari wameshakaribishwa! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:14, 17 Oktoba 2021 (UTC)Reply

Oh, my bad.
Sikujua nakosea, nashukuru kwa kunikumbusha hili. Wakati mwingine nitaweka kwenye majadiliano. Kuna namna ya kufuta hili kwenye kurasa zao? Aneth David (SLU) (majadiliano) 06:28, 21 Oktoba 2021 (UTC)Reply
Bila shaka. Ni kufuta tu, tena ukurasa wa mtumiaji hautakiwi kuingiliwa bila sababu kubwa. Amani kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:15, 21 Oktoba 2021 (UTC)Reply
Nimefuta kigezo kwa watumiaji ambao niliwawekea hivi karibuni. Asante sana kwa kunitaarifu hili.

Aneth David (SLU) (majadiliano) 08:59, 25 Oktoba 2021 (UTC)Reply

How we will see unregistered users

hariri

Hi!

You get this message because you are an admin on a Wikimedia wiki.

When someone edits a Wikimedia wiki without being logged in today, we show their IP address. As you may already know, we will not be able to do this in the future. This is a decision by the Wikimedia Foundation Legal department, because norms and regulations for privacy online have changed.

Instead of the IP we will show a masked identity. You as an admin will still be able to access the IP. There will also be a new user right for those who need to see the full IPs of unregistered users to fight vandalism, harassment and spam without being admins. Patrollers will also see part of the IP even without this user right. We are also working on better tools to help.

If you have not seen it before, you can read more on Meta. If you want to make sure you don’t miss technical changes on the Wikimedia wikis, you can subscribe to the weekly technical newsletter.

We have two suggested ways this identity could work. We would appreciate your feedback on which way you think would work best for you and your wiki, now and in the future. You can let us know on the talk page. You can write in your language. The suggestions were posted in October and we will decide after 17 January.

Thank you. /Johan (WMF)

18:19, 4 Januari 2022 (UTC)

Have you voted in the UCoC enforcement guidelines ratification?

hariri

Hi! @Asterlegorch367:

The ratification voting process for the revised enforcement guidelines of the Universal Code of Conduct (UCoC) is now open! Voting commenced on SecurePoll on 7 March 2022 and will conclude on 21 March 2022. Please read more on the voter information and eligibility details.

Please vote and encourage other editors of Swahili Wikipedia to also vote.

Regards, Zuz (WMF) (majadiliano) 12:29, 11 Machi 2022 (UTC)Reply

Matumizi ya FUTA

hariri

Habari naona umepeleka alama ya FUTA kwenye makala ya Risasi ya Danny Hansford (nakubali kabisa!). Ila: hujaingiza makala kwenye ukurasa "Wikipedia:Makala kwa ufutaji" . Isipopelekwa hapa, uwezekano ni mkubwa haitafutwa maana hakuna atakayeiangalia. Utaratibu mzuri ni: kuweka kifupi sababu za kupendekeza makala kwenye ukurasa wa majadiliano, halafu kopi maelezo hayo na kuyapeleka kwenye ukurasa wa ufutaji. Hadi sasa tunafuata utaratibu: mmoja anapendekeza, wingine yeyote anafuta; labda isipokuwa si makala kweli, ina matusi au machafuku matupu, hapo tunafuta pia mara moja. Kipala (majadiliano) 09:31, 5 Agosti 2022 (UTC)Reply

Asante sana, niliweka alama ya futa kwenye makala kama tatu, nilikua sikumbuki ukurasa wa Makala ya ufutaji. Nimeziweka sasa.
Asterlegorch367 (majadiliano) 10:22, 5 Agosti 2022 (UTC)Reply
Link ya ukurasa huo unatokea baada ya kuhifadhi sanduku ya FUTA kwenye ukurasa fulani. Mimi huweka kwanza sanduku la FUTA kwenye makala, halafu nakopi jina la makala na kufungua link ya ukurasa wa Ufutaji, na kuanzisha topic mpya... Kipala (majadiliano) 14:06, 5 Agosti 2022 (UTC)Reply

Ukumbusho kuhusu kupiga kura sasa ili kuchagua washiriki wa U4C ya awamu ya kwanza

hariri
Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language

Ndugu Mwanawikimedia,

Unapokea ujumbe huu kwa sababu hapo kabla uliwahi kushiriki katika mchakato wa UCoC.

Huu ni ukumbusho kwamba kipindi cha kupiga kura kwa Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) kitamalizika tarehe 9 Mei 2024. Soma maelezo kwenye ukurasa wa kupiga kura kwenye Meta- wiki ili kupata maelezo zaidi kuhusu upigaji kura na ustahiki wa mpiga kura.

Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) ni kikundi cha kimataifa kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii walialikwa kutuma maombi yao kwa U4C. Kwa maelezo zaidi na majukumu ya U4C, tafadhali pitia Mkataba wa U4C.

Tafadhali washirikishe ujumbe wanajumuiya wenzako ili nao waweze kushiriki.

Kwa niaba ya timu ya mradi wa UCoC,

RamzyM (WMF) 22:54, 2 Mei 2024 (UTC)Reply