Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Ndugu, naomba kujua tofauti kati ya Hip Hop ya Bongo na Hip Hop ya Tanzania. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:46, 5 Juni 2022 (UTC)Reply

salaam ndugu? sioni utofauti wa Hip Hop ya Bongo na Hip Hop ya Tanzania. Nilizitumia kama njia ya kupangilia makala vyema. Benix Mby (majadiliano) 15:27, 5 Juni 2022 (UTC)Reply
Wazo langu ni kuweka viungo vyote vinavyohusu Hip hop hapa Tanzania kwenye jamii ya "Hip Hop ya Bongo" na kutengeneza jamii ndogo ndogo mfano makundi, wasanii, albamu nk.‎ Benix Mby (majadiliano) 15:42, 5 Juni 2022 (UTC)Reply
Hatuwezi kuwa na jamii mbili zenye maana moja: mimi najua Bongo ni Dar, na Dar ni ndani ya Tanzania. Hivyo jamii Hip Hop ya Tanzania ni sahihi zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:43, 6 Juni 2022 (UTC)Reply
Riccardo, uko sahihi. Bongo ni Dar pekee. Tanzania ni nchi nzima.--Muddyb Mwanaharakati Longa 05:23, 25 Juni 2022 (UTC)Reply

Karibu!

hariri

Ndugu, kwema?

Naona nimepata mshirika kwenye uga wa hip hop ya Tanzania. Ni furaha yangu kuona makala za namna hiyo zinaboreshwa na kuongezeka pia. Sehemu kubwa ya matini ya Dizasta Vina ni nakala ya Nash MC. Kimsingi, tunahitaji makala nyingi zaidi lakini si za kufanana.

Pamoja sana mkuu! Muddyb Mwanaharakati Longa 05:35, 25 Juni 2022 (UTC) Reply

Asante kwa kunikaribisha. Nitafanya marekebisho kwenye makala ya Dizasta Vina. Pia nitaendelea kuboresha na kuongeza makala za namna hii. Asante!Benix Mby (majadiliano) 19:32, 1 Julai 2022 (UTC)Reply

Hongera

hariri

Nimefurahi kuona makala nzuri kuhusu TBC. Si kawaida kumpata mchangiaji mpya anayetunga makala ambayo ni safi kimaudhui na kiumbo. Hongera, tafadhali endelea! Kipala (majadiliano) 10:27, 1 Julai 2022 (UTC)Reply

Asante sana, nitajitahidi kuendelea kuboresha makala za Wikipedia kwa Kiswahili na kujifunza matumizi bora zaidi. Asante.Benix Mby (majadiliano) 19:22, 1 Julai 2022 (UTC)Reply

Kampuni

hariri

Ndugu, ilianza vema kutunga jamii kwa kutumia kampuni kama jina la wingi badala ya makampuni. Usirudi nyuma kwa kuweka makampuni. Kinyume chake, tunapaswa kubadilisha jamii zote ambazo zinataja makampuni tuweke kampuni tu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:23, 18 Agosti 2022 (UTC)Reply

Asante kwa maelekezo. Nafanya marekebisho sehemu zinazotaja makampuni.

Benix Mby (majadiliano) 09:36, 18 Agosti 2022 (UTC)Reply

tengeneza kurasa za watengenezaji wa magari kwa kiswahili Wikipedia

hariri

@Benix Mby hujambo, Tafadhali unaweza kuunda kurasa hizi kwa watengenezaji hawa wa magari kwa Kiswahili Wikipedia:

  • Alfa Romeo
  • Buick
  • Chevrolet
  • Chrysler
  • Citroen
  • Dodge
  • Fiat
  • Ford
  • GMC
  • Honda
  • Hyundai
  • Jaguar
  • Kia
  • Lancia
  • Land Rover
  • Lincoln
  • Mahindra
  • Mazda
  • Mitsubishi
  • Nissan
  • Peugeot
  • Renault
  • SAAB
  • SEAT
  • Škoda
  • Suzuki
  • Tata

Ningewashukuru sana kama mtawaumba kwa vile sijui Kiswahili na ninatumia mfasiriRHAXHIJA (majadiliano) 20:42, 21 Agosti 2022 (UTC)Reply

@Benix Mby Je, unaweza kuziunda tafadhali?

Kidogo nilikuwa nje ya mtandao ila nitaanza kuunda makala hizi hii leo. Benix Mby (majadiliano) 05:27, 16 Septemba 2022 (UTC)Reply

@Benix Mby bado haujaunda nakala hizi kwa watengenezaji hawa wa magari

Tafsiri kompyuta

hariri

Benix naona ulitambua kwamba Upigaji risasi wa wingi ilikuwa tafsiri ya komyuta. Ombi langu: ukiona kwamba kasoro za makala ni nzito, uipendekeze kwenye orodha ya makala kwa ufutaji. Njia rahisi ni kutumia kigezo {{futa}} halafu bofya kiungo na kuandikisha makala huko. Ukiona mada inafaa (lakini huna muda kuisahihisha mwenyewe) unaweza kuandika: "Kasoro nzito, iboreshwe au kufutwa". Kipala (majadiliano) 21:54, 7 Septemba 2022 (UTC)Reply

Asante kwa maelekezo ndugu Kipala.

Benix Mby (majadiliano) 07:38, 8 Septemba 2022 (UTC)Reply