Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 17:47, 30 Novemba 2009 (UTC)Reply

Jumuiya ya Afrika Mashariki

hariri

Salam, Earnest. Makala husika na kichwa cha habari hapo juu, ni makala uliyeanzisha nzuri mno. Hivyo, hongera! Nimesawazisha masuala fulani-fulani na ukitaka kuuliza lolote, basi uliza! Karibu sana.--  MwanaharakatiLonga 11:49, 3 Desemba 2009 (UTC)Reply

Overwrite

hariri

Bwana Earnest, salaam! Uliweka makala manne kwenye wikipedia. Kwa bahati mbaya hujafuata maagizo ya wikipedia:mwongozo hujatazama kabla ya kuandika kama makala iko tayari. Maana hapa wikipedia hatufuti kazi ya wengine bila kutaja kwanza sababu na kutafuta majadiliano kwa sababu hii ni sababu ya kuwa na ukurasa wa majadiliano. (Isipokuwa kama makala iliyopo inaonekana haifai kabisa, au ni kifupi mno - hapa mabadiliko makubwa ya mara moja ni sawa).

Sasa makala zote nne ulizotunga zilikuwepo tayari na wewe hujatafuta majadiliano. Kwa bahati mabya ulifuta kazi ya awali bila taarifa.

  1. Kwa hiyo nimerudisha hali ya awali kwa makala za Afrika na mfalme.
  2. Jumuiya ya Afrika Mashariki iko tayari kwa jina la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Naona mpangilio wa makala iliyopo ni afadhali lakini tafsiri yako ina habari za nyongeza. Hii ni nafasi nzuri ya kuongeza sehemu zisizotajwa bado.
  3. Biashara ilikuwepo tayari lakini kama makala fupi sana ya mbegu (mistari miwili pekee). Kwa hiyo ni sawa kuandika upya kabisa. Ila tu kuna mawili: a) ulibadilisha maana ya "biashara" - ilikuwepo kwa maana ya kazi ya kununua na kuuza "trade") - wewe ulitafsiri "business" kwa maana ya duka au kampuni. Je ulitazama viungo vyake kama bado sawa? Sijachungulia lakini itakuwa afadhali kuhamisha yote kwenda "Kampuni ya biashara".

b) makala jinsi iliyo haipendezi bado maana lugha inaonyesha asili katika programu ya google translate (yaani sentensi zisizo Kiswahili bado) na kuna viungo vingi mno vya rangi nyekundu vingine vya ajabu kama "ya uchimbaji madini" (hakuna atakayeandika makala kwa jina hii). Hii makala bado ina kazi ndani yake hadi kuwa makala nzuri. --Kipala (majadiliano) 09:12, 8 Januari 2010 (UTC)Reply

Your account will be renamed

hariri

08:27, 20 Machi 2015 (UTC)

Renamed

hariri

11:57, 19 Aprili 2015 (UTC)