Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:24, 23 Aprili 2022 (UTC)Reply

Maboresho ya Makala hariri

Salami! kelvin hongera kwa kuendelea na uhariri katika wikipedia Ya Kiswahili, baada ya kumaliza kuandika makala yako,baada ya muda fulani pitia katika makala yako ama pitia ukurasa wa Mabadiliko ya karibuni ili kuona makala yako imefanyiwa marekebisho gani, kisha tumia marekebisho hayo kama maboresho kwa makala zako nyingine, Amani sana Hussein m mmbaga (majadiliano) 19:48, 23 Aprili 2022 (UTC)Reply

Sawa mkuu, Kazi Iendelee Kelvin-Meena (majadiliano) 20:00, 23 Aprili 2022 (UTC)Reply

Tafsiri hariri

Salamu, pitia katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Safy_Boutella kuna dalili ya kutumia tafsiri ya kompyuta, ni heri kuifanyia marekebisho makala hii na makala nyingine ulizoanzisha kabla ya kuendelea, kwani kuendelea kuleta makale zenye tafsiri ya kompyuta kutapelekea kufungiwa, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 21:24, 23 Aprili 2022 (UTC)Reply

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Angalia pia katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Youssef_Alimam , makala imekuwa ni ngumu kueleweka, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 21:48, 23 Aprili 2022 (UTC)Reply


Tafsiri hariri

Bado katika makala zako kuna dalili nyingi ya uwepo wa matumizi ya mashine katika tafsiri, tafsiri zako bado hazieleweki. jaribu kupitia kwanza makala zako ulizoandika ili kuzifanyia marekebisho kulikoe kuendelea kuleta makala ambazo zinachangamoto ya kutokuwa na Kiswahili kinachoelewa,pia tazama namna makala nyingine zilivyoandikwa,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 09:31, 25 Aprili 2022 (UTC)Reply

Kwa kuwa husikii, leo nakuzuia kwa siku 3. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:17, 15 Mei 2022 (UTC)Reply
Kwa kuwa husikii, leo nakuzuia tena kwa siku 3. Pole na amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:42, 24 Mei 2022 (UTC)Reply

Makala ya Haki za Binadamu hariri

Salamu Kelvin, kama unashiriki katika shindano la Makala za Haki za Binadamu, basi usiende katika makala za zamani na kuziwekea jamii za ambayo ni kwa ajili ya Makala mpya ya Haki za Binadamu,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 08:26, 27 Mei 2022 (UTC)Reply
Sawa, Nimeelewa Kelvin-Meena (majadiliano) 09:50, 27 Mei 2022 (UTC)Reply
:Tazama katika makala hii hapa https://sw.wikipedia.org/wiki/Haki_za_wanawake_nchini_Saudi_Arabia , makala zako bado zina vyanzo vinavyotokana na link za Wikipedia ya Kiingereza, vyanzo vya aina hiyo havitakiwi katika Wikipedia ya Kiswahili,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 12:48, 30 Mei 2022 (UTC)Reply

Mipira ya samaki hariri

Salamu Kelvin. Ukianzia makala mapya tafadhali fuata mabadiliko katika makala haya na soma majadiliano yake. Niliweka maoni yangu na swali kwenye Majadiliano:Mipira ya samaki (angalia hapo chini). Bado ninangoja jibu lako.

Mipira wa samaki ni tafsiri isiyofaa kwa "fish balls". Maana ya mpira kwanza ni "rubber", kwa hivyo ikiwa maana yake ni "ball" hiyo ball ni aina ya rubber au labda ya plastiki. Kwa ujumla, "food ball" ni tonge kwa Kiswahili, au kitonge ikiwa ni dogo. "Meat ball" ni kababu, kwa hivyo labda tutumie hii kwa "fish ball" pia. Mnapendelea neno gani? ChriKo (majadiliano) 05:56, 22 Juni 2022 (UTC)Reply

Sawa Uko sahihi sana, Ahsante kwa marekebisho haya. "Fish ball" ingekuwa kababu za samaki? Kelvin-Meena (majadiliano) 15:49, 23 Juni 2022 (UTC)Reply
Sawasawa, kababu za samaki ni upendeleo wangu. ChriKo (majadiliano) 15:56, 23 Juni 2022 (UTC)Reply
Sawa Ahsante, Je inawezekana Kubadilisha Kichwa cha makala ambayo imeshaanzishwa tayari? Kelvin-Meena (majadiliano) 15:59, 23 Juni 2022 (UTC)Reply