Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 21:53, 30 Januari 2010 (UTC)Reply

Kunguru hariri

Mwasapi salaam. Nimeona hivi sasa uhariri wako wa ukarasa wa Kunguru. Tafadhali ukiongeza matini kwa ukarasa wo wote usiyaongeza kwa mwisho wake tu lakini yaunganishe kuwa ndani ya matini yanayowepo. Pia soma kurasa za msaada ili kupata kanuni za kutia viungo na tanbihi. Kila la heri! ChriKo (majadiliano) 00:36, 31 Januari 2010 (UTC)Reply

Mwewe hariri

Mwasapi, ndege ambao ulieleza katika ukurasa wa mwewe wanaitwa kipanga (Accipiter, Urotriorchis, Megatriorchis), kizu (Micronisus, Melierax), koho (Pandion) na shakivale (Buteo) kwa Kiswahili. Waeleze katika kurasa zao.ChriKo (majadiliano) 12:28, 31 Januari 2010 (UTC)Reply

Nguruwe hariri

Mwasapi kihongosi, nimeangalia nyongeza zako katika makala "nguruwe". Nikihisi vema umefanya kazi kwa msaada wa google-translate? Napenda kukupongeza kwa sababu uanandika kiswahili kizuri na cha kueleweka (bahati mbaya kwa washiriki wengi wa mashindano matokeo yalikuwa ya kuhuzunisha). Pia nakupongeza kwa kutofuta maandishi ya awali tu (jinsi wengi walifanya kwa kutojua), Je wewe unasoma somo linalohusiana na biolojia?

Kuhusu mpangilio wa makala kuna bado kazi. Umeweka YOTE CHINI ya maandishi yaliyokuwepo. Hapa hatuna budi kulinganisha yale yaliyopo na yale tuliyoandaa. Maana sasa kuna mambo yanayorudia. kama yale yaliyopo hayana kosa ni ungwana wetu kuyaacha kwa heshima kwa wale waliotangulia. (wakati mwingine ni lazima kuandika yote upya...)

Sasa mambo yanarudiarudia. Sijui kama bado upo baada ya shindano lakini naomba uangalie makala na fanya usafi yaani kuangalia mpangilio. Ningefurahi kama unaendelea maana una lugha nzuri na unaonekana unajua kitu. Nimeona kwenye makala ya tembo ni hali ileile; nafurahi sana ukichukua muda kuangalia makala hizi upya!

Mwisho: Usione aibu kujibu hapa au katika ukurasa wangu au kwa ChriKo - ni kawaida yetu! --Kipala (majadiliano) 07:20, 13 Februari 2010 (UTC)Reply