Salaam. Sikiliza ndugu. Jitahidi ufuate utaratibu wetu na si hivyo ufanyavyo. Unadhani nisingefahamu kama wewe ni Lusajo? Usihamishe makala ambazo zipo tayari na kuzipeleka katika majina unayoyataka wewe. Ukiendelea hivyo, nitakuwa ninakuzuia kila uhamiapo hadi utakapoacha. Hapa si mahali pa kusema uwongo.--MwanaharakatiLonga 07:31, 22 Juni 2015 (UTC) Reply

nimekuelewa hapo
Ukiwa umeelewa, mbona unaendelea kuingiza habari kuhusu kilabu na wachezaji wasio na umaarufu wa kutosha? Mechi za kilabu hazifai kwa kamusi elezo. Wikipedia siyo chombo cha habari za kila siku! Michango hiyo yatafutwa moja kwa moja. Naomba ufuate kanuni za Wikipedia:Umaarufu! --Baba Tabita (majadiliano) 15:45, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Soma ukurasa wa msaada kuhusu umaarufu

hariri

Ndugu, naomba usome ukurasa wa Wikipedia:Umaarufu. Halafu utaelewa sababu ya maombi ya kufuta makala za wachezaji wa kilabu cha Black Leopards Under 20 huko Mbalizi (angalia Wikipedia:Makala kwa ufutaji). Karibu kuchangia habari ambazo zingefaa kwa kamusi elezo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 17:48, 28 Juni 2015 (UTC)Reply

Makala kwa ufutaji

hariri

Bwana, unapoteza muda wako. Michango yako yote hayafai kwa kamusi elezo kwa vile watu hawa hawana umaarufu wa kutosha. Angalia Wikipedia:Makala kwa ufutaji ili uelewe sababu za mapendekezo ya kufuta makala hizo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 15:51, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Ndugu Oliver, unajisumbua tu.. Nimeshatimiza azma ya matendo yake katika akaunti ile nyingine.. nadhani na humu si muda mrefu litamfika!--MwanaharakatiLonga 16:06, 29 Juni 2015 (UTC)Reply
Asante, Ndg Muddyb, kwa mashauri yako. Nimewauliza wazee wetu watatu wanaonaje Silausi akiendelea bila kufuata kanuni za wikipedia. Kweli, litamfika asipobadilisha mwenendo ... --Baba Tabita (majadiliano) 16:51, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Naomba utafakari kidogo

hariri

Mpendwa nimewahi kukuandikia. Hii si wikipedia yangu (kama kama mimi ni mratibu hapo) na inasubiri kuwa wikipedia yako. KAMA uko tayari kuelewa na kuitikia kanuni za kimsingi. Hapo tumejaribu kukusaidia, kwa wiki kadhaa hujafuata. Sina uhakika ni kiasi gani kutoelewa na kiasi gani kiburi. - Unapenda kujiweka menyewe na kundi lako la vijana katika intaneti. Basi hii ni kawaida kwa wageni wengi wanaoanza hapa. Lakini wewe hadi sasa hujaonyesha ya kwamba wewe u mtu anayestahili makala (na mimi mwenyewe sina makala hapa!). Kwa hiyo hutapata makala wala watoto wenzako.

LAKINI kama unapenda kuchangia kuhusu mpira wa miguu na michezo nitakupokea kwa mikono yote miwili! Nina uhakika ya kwamba unajua mambo hayo kushinda mimi. Kuhusu umbo la makala unahitaji kujifunza bado unarudia makosa yaleyale niliyokueleza. Dawa lake ni KUULIZA. Utapata jibu na sisi sote hapo tumeulizana na kufundishana.

Kwa hiyo TAFAKARI: Ukiendelea kama ulivyofanya utafungwa hata kwa majina mengine (tuna teknolojia ya global blocking kwa kila IP). Ukianza kuuliza kuhusu kanuni na namna ya kuhariri tutafurahia kutoa maelezo na kusoma michango yako. Chaguo ni lako! Kipala (majadiliano) 19:28, 29 Juni 2015 (UTC)Reply

Labda nimpe pendekezo la mwisho.. Naomba unipigie simu namba 0713-53-84-27 kwa vile tupo nchi moja nitakueleza ana-kwa-ana jinsi ya kuandika makala. Bado tunahitaji msaada wako, ila tu hujui namna ya kufanya. Fanya hivyo kisha tuone nini tunafanya.--MwanaharakatiLonga 11:51, 30 Juni 2015 (UTC)Reply

Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima

hariri

Naomba usome ukurasa wa majadiliano wa makala hii ukasahihishe. Kipala (majadiliano) 08:06, 3 Septemba 2015 (UTC)Reply


Nadir haroub Ali

hariri

habari Silausi, naomba uangalie nilichoandika katika ukurasa wa majadiliano . Kuna kasoro kadhaa naona afadhali upate kuisahihisha mwenyewe! Itakusaidia kwa makala nyingine. Asante --151.242.139.148 19:13, 22 Aprili 2016 (UTC)Reply

Hans van der Pluijm‎

hariri

Naona sasa kuna sehemu za makosa yaleyale katika makala ya Hans van der Pluijm. Naomba pitia tena na kusahihisha. --Kipala (majadiliano) 19:56, 22 Aprili 2016 (UTC)Reply

ans van der Pluijm‎

hariri

Naona sasa kuna sehemu za makosa yaleyale katika makala ya Hans van der Pluijm. Naomba pitia tena na kusahihisha. --Kipala (majadiliano) 19:56, 22 Aprili 2016 (UTC)Reply