Majigambo
Majigambo ni masimulizi ya kujigamba/kujitapa/kujisifu kwa mtu kuhusu matendo ya kishujaa aliyoyatenda katika maisha yake. Majigambo hayo husimuliwa kwa lugha ya kishairi na masimulizi yake huambatana na vitendo vya anayejigamba. Majigambo hujulikana pia kama "vivugo".
Majigambo hufanyika pindi mtu anapokuwa amefanya jambo kubwa la kishujaa kama vile: kuua simba, kuua adui, kulima shamba kubwa n.k.
Jamii nyingi, hufanya sanaa hii kwa lengo la kujengana ari katika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika maisha yetu ya kila siku.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Majigambo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |