Chuo Kikuu cha Makerere
Chuo Kikuu cha Makerere ni chuo kikuu cha kwanza cha Afrika ya Mashariki na chuo kikuu kikubwa cha Uganda.
Makerere University | |
---|---|
Chuo Kikuu cha Makerere | |
Wito | We Build for the Future |
Kimeanzishwa | 1922 |
Aina | umma |
Chansela | Ezra Suruma |
Mahali | Kampala, Uganda |
Kampasi | mjini Kampala |
Tovuti | http://www.mak.ac.ug |
Kimeanzishwa wakati wa ukoloni mwaka 1922 kama shule ya ufundi kwa wanafunzi 14. Kozi za kwanza zilikuwa pamoja na useremala, ujenzi na umekanika.
Shule ikawa chuo na kozi zikaongezeka kwa masomo ya utabibu, kilimo, maradhi ya wanyama na ualimu.
Kuanzia mwaka 1937 chuo kilianza kozi za stashahada mbalimbali.
Mwaka 1949 Makerere ikawa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha London kikitoa shahada ya kwanza ya ngazi ya chuo kikuu.
Mwaka 1963 ikawa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki pamoja na kampasi za Dar es Salaam na Nairobi.
Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kimegawiwa mwaka 1970 kutokana na kufifia kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makerere ikawa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Uganda.
Chuo cha Viongozi
Makerere ilikuwa chuo waliposoma viongozi wengi wa Afrika, wakiwa pamoja na marais wa zamani Milton Obote (Uganda), Julius Nyerere na Benjamin Mkapa (Tanzania) na Mwai Kibaki (Kenya).
Baada ya uhuru Makerere ilikuwa pia mahali pa majadiliano na mafunzo ya utamaduni wa Kiafrika. Waandishi na walimu muhimu wa Kiafrika walianzisha mafunzo yao au walifundisha kwa muda fulani Makerere kama vile Nuruddin Farrah, Ali Mazrui, David Rubadiri, Okello Oculi, Ngugi wa Thiongo, John Ruganda, Paul Theroux na Peter Nazareth.
Idara
Makerere ina idara 22 zinazohudumia wanafunzi 30,000 hivi, wakiwemo 3,000 wa kozi za shahada za ngazi ya juu.
Vitivo
- Kitivo cha Kilimo
- Kitivo cha Fani
- Kitivo cha Elimu Misitu na Hifadhi la Mazingira
- Kitivo cha Sheria
- Kitivo cha Uganga
- Kitivo cha Sayansi
- Kitivo cha Sayansi Jamii
- Kitivo cha Teknolojia
- Kitivo cha Elimu ya Maradhi ya Wanyama
Taasisi
- Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
- Taasisi ya Sayansi ya Kompyuta
- Taasisi ya Uchumi
- Taasisi ya Mazingira na Mali Asili
- Taasisi ya Uchunguzi wa Kijamii
- Taasisi ya Takwimu na Saikolojia
Vyuo
- Chuo cha Ualimu
- Chuo cha Sanaa
- Chuo cha Sayansi za Maktaba na Habari
- Chuo cha Biashara
- Chuo cha Mafunzo baada ya Digrii ya Kwanza
Idara
- Idara ya Teknolojia ya Kompyuta na Habari
Kampasi
- Makerere - Kikara
- Makerere - Kabanyoro
- Makerere - Katumani
Wanafunzi waliopitia Chuo Kikuu cha Makerere
- John Sentamu, Askofu Mkuu wa York, askofu mkuu Mwafrika wa kwanza katika Kanisa la Uingereza
- Okello Oculi, mwandishi, mshairi
- Peter Nazareth, mwandishi
- David Rubadiri, mwandishi na mshairi wa Malawi
- Benjamin Mkapa, alikuwa rais wa Tanzania
- Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Specioza Kazibwe, mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Uganda (1994-2003)
- Julius Nyerere, alikuwa rais wa Tanzania
- Milton Obote, alikuwa rais wa Uganda
- Sir Frederick Edward Mutesa II, alikuwa Kabaka wa Buganda
- Mwai Kibaki, alikuwa rais wa Kenya (alikuwa pia mwalimu Makerere)
- Ngugi wa Thiongo, mwandishi (alikuwa pia mwalimu Makerere)
- Jaramogi Oginga Odinga, mwanasiasa na makamu wa rais wa Kenya (1964-1966)
- Okot p'Bitek, mshairi na mwandishi (alikuwa pia mwalimu Makerere)
- Chege Joseph Macharia, mwalimu wa Kiswahili
- Don Gasangwa, siasa ya Eacu
- Helen Akwi, mwandishi wa hadithi
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Tovuti rasmi