Makumbusho ya Taifa ya Gitega
Makumbusho ya Taifa ya Gitega (kwa Kifaransa: Musée National de Gitega, kwa Kirundi: Iratiro ry'akaranga k'Uburundi) ni makumbusho ya taifa yaliyopo nchini Burundi. Ndiyo makumbusho makubwa nchini Burundi [1].
Makumbusho hayo hupatikana katika eneo la Gitega na yalianza kutumika wakati wa utawala wa wakoloni Wabelgiji mwaka 1955.[2]
Mwaka 2014 makumbusho hayo yalitembelewa na watu 20 hadi 50 kwa wiki.[3]
Makumbusho hayo yalijengwa kwa ajili ya kutunza utamaduni wa Warundi ambao ulikuwa unaelekea hatarini kutokana na muingiliano na jamii nyingine, makumbusho yakikusanya kazi nyingi za kitamaduni na kisanaa zikiwemo zile za ufalme wa Burundi.
Mwaka 2015, orodha ya makusanyo katika makumbusho hayo, yalichapishwa na ubalozi wa Ujerumani kwa jina la Le Patrimoine Burundais: le Musée de Gitega.[4]
Marejeo
hariri- ↑ "Musée national de Gitega". Lonely Planet. Iliwekwa mnamo 5 Januari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Burundi - Libraries and museums
- ↑ Irambona, Yvette. "Musée national de Gitega: Etat des lieux". Publication de Presse Burundaise. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-06. Iliwekwa mnamo 5 Januari 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Un livre pour immortaliser la richesse du Musée national de Gitega", IWACU: Voix du Burundi, 25 January 2015. Retrieved on 5 January 2017.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Makumbusho ya Taifa ya Gitega kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |