Maporomoko ya Huangguoshu

Maporomoko ya Huangguoshu ni mojawapo ya maporomoko maarufu yenye maajabu zaidi duniani. Maporomo ya Huangguoshu yanapatikana bara la Asia nchini China: ni mojawapo ya maporomoko 18 yanayopatikana huko China sehemu inayoitwa Guizhou.

Maporomoko yalivyo.

Asili ya neno Huangguoshu ni matunda ya kimanjano yanayopatikana hasa huko China.

Maporomoko haya yana urefu wa mita zipatazo 75 yakitiririka kutoka juu kileleni mwa miamba na kumwagika chini kabisa katika mito mingine midogomidogo. Hiki ni kivutio cha ajabu ambacho watalii wengi hustaajabu na kuvutiwa nacho, kitu cha pekee katika maporomoko ya Huangguoshu ni kuwa maji na mawe hugusana na kugongana kwa nguvu sana kiasi ambacho hutoa sauti ya ngurumo. Hata hivyo, juu kileleni mwa miamba kuna mawingu ambayo watu wakikaa mita 50 hadi 60 hujikuta wakilowana chapa chapa bila kumwagiwa maji yatiririkayo katika maporomoko hayo.

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maporomoko ya Huangguoshu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.