Mariano Díaz

(Elekezwa kutoka Mariano)

Mariano Díaz Mejía (matamshi ya Kihispania: [maɾjano ði.az mexi.a]; anajulikana sana kama Mariano; alizaliwa Agosti, 1993, ni mchezaji wa soka wa Hispania anayecheza kwenye klabu ya Real Madrid kama mshambuliaji.

Mariano Díaza(Nyeupe)

Kazi ya klabu hariri

Muda mfupi baada ya kuanza katika klabu ya Badalona mwaka 2011, Mariano alijiunga na Real Madrid, ambako alicheza katika timu C ambapo alikuwa mchezaji bora katika daraja hilo msimu wa 2015-16.

Olympique Lyonnais hariri

Tarehe 30 Juni 2017, Mariano alisajiliwa na klabu ya Olympique Lyonnais.Kwa malipo yaliripotiwa kuwa ni milioni 8 .Alicheza kwa mara ya kwanza 5 Agosti katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2017-18 Ligue 1 dhidi ya klabu ya Strasbourg, akifunga magoli mawili katika ushindi wa nyumbani kwa magoli 4-0.

Alifikisha magoli 18 kwa msimu wa ligi, na kutengeneza nafasi kubwa ya kuwa mshambuliaji bora pamoja na Memphis Depay na Nabil Fekir.

Rudi Real Madrid hariri

Tarehe 29 Agosti 2018, Real Madrid ilitangaza kwamba walikuwa wameshamsaini Mariano kwa mkataba wa miaka mitano (5) kwa ada isiyopungua € 23,000,000.] Alipewa jezi nambari 7 iliyokuwa imevaliwa na Cristiano Ronaldo.

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mariano Díaz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.