Marselino wa Embrun

Marselino wa Embrun (alifariki Embrun, leo nchini Ufaransa, 374) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo kuanzia mwaka 354[1] alipowekwa wakfu na Eusebi wa Vercelli.

Mzaliwa wa Afrika Kaskazini, alikwenda Roma mwaka 313 kushiriki sinodi dhidi ya Wadonati akatumwa na Papa Miltiades huko Ufaransa alipoinjilisha sehemu mbalimbali hadi Italia Kaskazini[2].

Alifanikiwa kiasi kwamba alipofariki halikuwepo tena hekalu lolote la Kipagani katika jimbo lake[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Aprili[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Saint Marcellin d'Embrun.
  2. Jacques Humbert (1972). Embrun et l'Embrunais à travers l'histoire. Société d'études des Hautes-Alpes. uk. 49.
  3. Albert, Antoine (1783). Histoire Géographique, Naturelle, Écclésiastique Et Civile Du Diocese D'Embrun. Juz. la Tome I. uk. 53.
  4. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.