Eusebius wa Vercelli

Eusebius wa Vercelli (kisiwa cha Sardinia, 2 Machi 283 hivi – Vercelli, Piemonte, 1 Agosti 371) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika karne ya 4, wa kwanza katika mji huo wa Italia Kaskazini.

Bikira Maria katika utukufu pamoja na Malaika Gabrieli, na watakatifu Eusebius wa Vercelli (ameketi), Sebastiano na Roko katika mchoro wa Sebastiano Ricci.
Sehemu ya Codex Vercellensis, inayodhaniwa kuwa iliandikwa na Eusebius mwaka 370.

Alikusanya mapadri wa jimbo lake kuishi kimonaki na kuimarisha Ukristo katika eneo lote karibu na milima ya Alpi.

Pamoja na Atanasi wa Aleksandria alitetea imani katika umungu wa Yesu dhidi ya Waario na kwa ajili hiyo aliteswa na kupelekwa na kaisari Konstans uhamishoni Palestina, Kapadokia na hadi jangwa la Misri.

Miaka 8 baadaye aliweza kurudi jimboni mwake akaendelea na umisionari wake pamoja na kuimarisha waumini katika imani sahihi [1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 2 Agosti[2].

Tazama pia

hariri

Maandishi yake

hariri
  • Toleo jipya la maandishi yake linapatikana katika gombo la 9 la Corpus Christianorum - Series Latina.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • N. Everett, "Narrating the Life of Eusebius of Vercelli", in R. Balzaretti and E.M. Tyler (eds), Narrative and History in the Early Medieval West (Turnhout, 2006: Brepols), pp. 133–165.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.