Mathayo I wa Aleksandria

Mathayo I wa Aleksandria kuanzia mwaka 1378 hadi 1408 alikuwa Patriarki wa 87 wa Wakopti[1].

Msalaba wa Kikopti.

Akiwa na umri wa miaka 14 alijiunga na monasteri na kufikia miaka 18 alipewa upadrisho.

Alisaidia kujulisha Waislamu kwamba Wakristo wa Misri hawahusiki na maovu ya wenzao wa Ulaya wakati wa Vita vya msalaba.

Alipochaguliwa kuwa Papa wa Aleksandria alianza kujiita El Meskin ("Maskini") akawa na misaada mikubwa kwa mafukara pamoja na kuendelea kutetea Wakristo dhidi ya dhuluma za kidini.

Anaheshimiwa na Wakopti kama mtakatifu.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Coptic synexarium. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-06-11. Iliwekwa mnamo 2018-03-07.
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.