Matumizi ya Lugha
Makala hii au sehemu ya makala hii inahitaji masahihisho kwa upande mmoja wa zifuatazo:
|
Matumizi ya lugha hutahini uwezo wa mwanafunzi wa kuelewa na kukitumia Kiswahili kwa kuongea na kuandika.
Vipashio vya lugha
Lugha huundwa na:
Sauti za Kiswahili
Huwa mbili:
- i. Irabu
- ii. Konsonanti
-->Irabu ni tano. (a, e, i, o, u)
Irabu na Konsonanti (Matamshi na aina)
Unapotamka irabu, hakuna hewa inayozuiliwa lakini konsonanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa na ala za matamshi.
Kutamka Irabu(ulimi na midomo hutumika)
--e, i: Ni za mbele ya ulimi, midomo imetandazwa.
--a : Ni ya kati ya ulimi, midomo imetandazwa, ulimi huinuka na kutandazwa.
--o, u: Ni za nyuma ya ulimi, midomo imeviringwa.
>>Aina za Konsonanti
- a. Vipasuo: p, b, k, g, d, t
- b. Ving'ong'o/nazali: m, n, ng', ny
- c. Vikwamizi: dh, f, gh, h, s, sh, th, v, z
- d. Kitambaza: l
- e. Kimadende: r
- f. Viyeyusho: y, w
- g. Kizuio-kwamizo: ch
Silabi mwambatano
Mifano ya silabi mwambatano: --bw: bwaga, bweka --nd: ndimu, ndoa, ndugu
Kuchanganua Sentensi (sawa na kupambanua/kuainisha)
Kuna njia tatu:
- i. Kutumia matawi
- ii. Kutumia mishale
- iii. Kutumia sanduku/jedwali
Matumizi ya PO
- i. Kuonyesha wakati
Mfano: Alipoenda alikuwa amechelewa.
- ii. Kuonyesha mahali
Mfano: Hapo pananuka.
Matumizi ya KWA
- a. Kuonyesha mahali
Hadija yuko kwa Mwangi.
- b. Kuonyesha chombo cha utendaji
Alisafiri kwa basi
- c. Jinsi
Alimfokea kwa ghamidha
- d. Umilikaji wa mahali
Hujafika kwao.
- e. Kuonyesha uhusiano wa sehemu ya kitu kizima
- f. Kuleta dhana ya swali
Ni kwa nini umetenda haya?
- g. Kuonyesha muda ambapo jambo lilitendeka
Alifungwa jela kwa miaka kumi.
- h. Sababu/nia
Aliadhibiwa kwa utundu wake.
- i. Kuonyesha mfululizo wa utendaji wa jambo
i.Ujumbe ule ulipelekwa moja kwa moja ii.Walikaa sako kwa bako.
- j. Kuonyesha matokeo ya jambo
Alisoma kwa hivyo akapita mtihani
- k. Kuonyesha muda
Alikaa huko kwa muda wa siku nyingi.
- l. Kama kilinganishi
Walipata magoli matano kwa nunge.
i.Kuonana uso kwa uso ii.Beba kwa bega