Melesi wa Antiokia

Melesi wa Antiokia (Malatya, Armenia ya Kale, karne ya 3 au karne ya 4 - Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 381) alikuwa askofu mkuu wa Antiokia, leo nchini Uturuki, kuanzia mwaka 360 hadi kifo chake, ingawa alifukuzwa mara tatu na makaisari waliounga mkono Uario[1].

Picha takatifu ya Mt. Melesi wa Antiokia.

Alifariki akiwa anasimamia mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli.

Gregori wa Nisa na Yohane Krisostomo walimsifu sana kwa maadili yake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kwenye 12 Februari[2][3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Cavallera, F. Le Schisme de Mélèce. Paris: Picard, 1906.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.