Menelik II.
Menelik II (17 Agosti 1844 – 12 Desemba 1913) alikuwa mfalme mkuu wa Uhabeshi kutoka 1889 hadi 1913. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Sahle Miriam.
Alikuwa mtemi (Ras) wa jimbo la Shoa kati ya 1865-1889. Akashinda katika mvurugo baada ya kifo cha Yohane IV kwa msaada wa Italia akakubaliwa mfalme mkuu wa Ethiopia mwaka 1889.
Alikataa madai ya Italia kutokana na mkataba wa Wuchale. Mwaka 1896 alishinda jeshi la Italia katika mapigano ya Adowa. Ushindi huu ulihakikisha uhuru wa Ethiopia kama nchi ya pekee katika Afrika nje ya Liberia.
Menelik aliweka misingi ya maendeleo ya Ethiopia kuwa nchi ya kisasa lakini hakubadilisha muundo wa utawala wa kimakabaila.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Uhabeshi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Menelik II. kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |