Metafizikia ni tawi la falsafa linalochunguza asili msingi ya ulimwengu.

Konfutsu, mwanafalsafa wa China.

Kifupi, metafizika inajaribu kujibu hasa maswali mawili: 1. nini kipo? 2. kama kipo, kinakaaje?

Hivyo, mada za uchunguzi za wanametafizikia ni kama vile: uwepo, vitu na sifa zake, nafasi na wakati, usababishi na uwezekano.

Tawi kuu la metafizika ni ontolojia, uchunguzi wa makundi ya kuwepo na namna yanavyohusiana.

Wanafalsafa kadhaa na wanasayansi, kama vile wanamantiki chaya, wametupilia mbali somo zima la metafizikia na kusema halina maana, lakini wengine wanakiri kuwa somo hili ni halali.

Etimolojia

hariri

Neno “metafizikia” limetokana na maneno ya Kigiriki: μετα meta (“ng'ambo ya”, “juu ya” ama “baada ya”) na φυσίκή fysike (fizikia, uasilia). Ilitumika mara za kwanza kama kichwa cha maandishi kadhaa ya Aristoteli kwa umbo la μετὰ τὰ φυσικά meta ta fysika ng'ambo ya fizikia.

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metafizikia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.