Ahabu
(Elekezwa kutoka Mfalme Ahabu)
Ahabu (kwa Kiebrania: אַחְאָב, Aẖ'av, ʼAḥʼāḇ), mwana wa Omri, alikuwa mfalme wa saba katika ufalme wa Israeli. William F. Albright alikadiria utawala wake kuwa miaka 869–850 KK, E. R. Thiele miaka 874–853 KK[1] na Michael D. Coogan miaka 871–852 KK.[2].
Vitabu vya Wafalme vinamchora kama mwovu sana, kwa kufuata mke wake Yezebeli, kumuua Naboti na kuelekeza taifa la Israeli kuabudu miungu mingi, hasa Baali.
Lakini Nabii Elia kwa karama yake ya kutokea na kutoweka hakuweza kuuawa kama manabii wenzake wengi, akafaulu kuokoa imani katika Mungu pekee, YHWH.
Tanbihi
hariri- ↑ Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257.
- ↑ Michael D. Coogan, A Brief Introduction to the Old Testament, (Oxford: Oxford University Press, 2009) 237.
Marejeo
hariri- Craig, James A. "The Monolith Inscription of Salmaneser II." Hebraica 3,4 (1887): 201-232
Viungo vya nje
hariri- Ahab Ilihifadhiwa 14 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.—Archaeowiki.org
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ahabu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |