Yezebeli
Yezebeli (kwa Kiebrania אִיזֶבֶל|אִיזָבֶל |Izével|Izável|ʾÎzéḇel|ʾÎzāḇel) alikuwa malkia wa Israeli kama mke wa Mfalme Ahabu katika karne ya 9 KK.
Binti wa mfalme Ethbaal wa Tiro, Finisia, alimhimiza mumewe kuachana na imani ya taifa lake katika Mungu pekee, YHWH akaangamiza manabii wake (1Fal 16:21-31 ).
Aliyeokoa imani hiyo ni nabii Elia ambaye katika mlima Karmeli alishinda manabii wa miungu Baal na Ashera waliotunzwa na Yezebeli (1Fal 18).
Kazi yake ilikamilishwa na mwanafunzi wake, nabii Elisha aliyempaka mafuta Yehu awe mfalme na arudishe Israeli kwa Mungu wake. Katika mapinduzi yake, Yezebeli aliuawa kikatili (2Fal 9:1-36) kama alivyotabiri Elia.
Kwa uovu wake, Yezebeli anatajwa na Kitabu cha Ufunuo pia (2:20-23).
Tanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yezebeli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |