Nabii

(Elekezwa kutoka Manabii)

Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Nabii Isaya. alivyochorwa na Michelangelo katika Cappella Sistina, Vatikani.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Watu wa namna hiyo wanapatikana katika dini nyingi, hususan katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.

Katika Uyahudi

hariri

Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".

Katika Ukristo

hariri

Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.

Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Katika Uislamu

hariri

Katika Islam mtume Muhammad anapewa nafasi ya pekee kati ya manabii wengi waliotumwa na Mungu kwa binadamu wa nyakati na mahali tofauti. Ndiye anayesadikiwa na Waislamu wengi kuwa nabii wa mwisho na wa kudumu ("mhuri wa manabii" - khātim al-nabiyyīn (Kurani, XXXIII:40).

Uislamu unakubali manabii wa Biblia pamoja na wengine wasiotajwa katika kitabu hicho, kama vile Mwarabu Salih.

Katika dini nyingine

hariri

Dini nyingine zinatokana na mafundisho ya mtu anayehesabiwa nabii, kama vile: